ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 11, 2011

TAREHE 8MACHI MWANZA ILIVYO ADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Pamoja na kwamba tumeadhimisha miaka 100 ya siku ya wanawake duniani ikiwa ni nia ya kukomesha na kutokomeza vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa dada zetu na mama zetu.Mama huyu mwenye watoto watatu sikio lake hili pamoja na sikio la upande wa pili yamekatwa na mumewe katika ugomvi wa kifamilia na kumwachia ulemavu wa kudumu, mume anadai kuwa 'Ni mke wake amemtolea mahali hivyo atamfanya anavyotaka'.

Wakati hadhira ikiendelea kutafakari kuhusu kilichompata mwanamke huyo kwa kula burudani kutoka kundi la Bwela Masonga toka kata ya Kisesa binti wa miaka 13 ambaye sasa ni mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Isangijo, anasimulia kisa cha kuhuzunisha kilichompata kabla ya kupata msamalia mwema anayemsomesha sasa.Amekaa katika familia hiyo kwa muda wa miezi mi4, watoto wa familia hiyo wakiwa na kawaida ya kukojoa kitandani, Ikatokea siku moja naye akajikuta kakojoa kitandani, mwajiri wake akamwambia atamwonyesha gharama za ukojozi wake. Mwajiri huyo alichemsha kisu kwenye moto na kumchoma nacho sehemu za siri huku akimwonya ole wake akimwambia mtu.

Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Diwani wa viti maalum Hilda Komanya akipitia kipengere baada ya kipengere risala iliyosomwa.

Kwaya ya mazuzule ikitumbuiza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kijiji cha Isangijo wilayani Magu.

Kama ilivyo jamii nyingine kukusanyika katika maeneo mbalimbali duniani kuadhimisha siku hii na sasa maadhimisho yanatimiza miaka 100, kwa style hii jamii isipo badilika tutegemee kusherehekea miaka mingine 100 tukisimuliana mabaya zaidi ya haya tuyaonayo. 'Ukombozi lazima uanze na jamii'.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.