ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 11, 2011

MJI WA MAGU NA MAZINGIRA.

Hata wakazi wa town senta ya mji wa magu hutumia kuni kupikia na kuchemshia maji, ukosefu wa nishati mbadala sababu kubwa ya ukataji miti hovyo ndani ya hifadhi ya msitu wa Sakaya hali ambayo inatishia kukauka kabisa kwa mto Simiyu unaotiririsha maji yake ndani ya ziwa Victoria.

Bei ya kuku soko la Magu ni shilingi 4,000/= hadi 5,000/=

Ni asubuhi tuliiiiivu! pozi la kugombania magari barabarani 'Gari langu hilooo!' kutoka kushoto ni viongozi wetu wa kesho Simon, Jose, Charles na Jane.

Ni mwendo kulishwa kondoo kwa wanaoagiza supu hasa ya mbuzi. (limenitokea)

Mjini hapa ukiuliza daladala, basi utaelekezwa hapa. Nauli maelewano ni kati ya 100, 200 au 300 kutokana na umbali wa eneo hadi eneo, wala hazipandi kama zile za Sumatra.

Licha ya kuwa karibu na ziwa upatikanaji wa maji wilayani Geita bado Inshu'

Kanisa la Kakobe (full gospel) la mjini geita na utunzaji wa mazingira.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.