Katibu tawala wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Theresia Mtewele akimkabidhi Tuzo ya Walipakodi Bora kwa Wilaya ya Kasulu kwa mwaka wa fedha 2023/2024,Mshindi wa kwanza Kasulu Motel Co LTD kwa kuwa mlipa kodi mzuri
Katibu tawala wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Theresia Mtewele akimkabidhi Tuzo ya Walipakodi Bora kwa Wilaya ya Kasulu kwa mwaka wa fedha 2023/2024,Mshindi wa pili,Malagalasi Enterprises & Contractors Co. LTD
Katibu tawala wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Theresia Mtewele akimkabidhi Tuzo ya Walipakodi Bora kwa Wilaya ya Kasulu kwa mwaka wa fedha 2023/2024,Mshindi wa tatu,Zabron Nashon Baroshigwa Co. LTD
Na Fredy Mgunda, Kigoma.
Wafanyabishara wa Mkoa wa Kigoma wameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuendelea kutoa elimu ya mlipa Kodi iliyopelekea wafanyabishara kulipa kodi kwa wakati na kwa haki na kupunguza utitiri wa Kodi.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo Walipa Kodi wazuri kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Kirahumba Kivumu mfanyabiashara aliyenyakua tuzo Bora ya mlipa Kodi Mkoa wa Kigoma alisema kuwa kwa sasa kulipa kodi limekuwa suala la kukaa mezani na kujadiliana sio vita tena kama inavyodhaniwa hapo awali na kuwaomba wafanyabishara kutunza kumbukumbu pamoja na kutoa lisiti wanapouza bidhaa na wateja kudai risiti wanaponunua bidhaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabishara Mkoa wa Kigoma Bw. Juma Chaulembo alipongeza mfumo mzima wa ulipaji kodi kuwa umesaidia kuondoa utiti wa kodi na kuwa rafiki kwa wafanyabishara wa Mkoa huo na kupongeza juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukuza uchumi wa Wafanyabishara wa Mkoa wa Kigoma.
Beatus Nchota ni Meneja wa TRA Mkoa wa Kigoma aliwapongeza wafanyabishara wote kwa kuendelea kulipa kodi kwa wakati na haki na kuiunga mkono Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika suala la ukusanyaji wa mapato uliopelekea kukusanya bilioni 15.48 kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Naye Bi. Julieth Nyomolelo mwakilishi wa Kamishina Mkuu wa TRA alisema kuwa tuzo hizo zinalengo la kuwaongezea morali wafanyabishara kulipa kodi kwa wakati na haki ili kuchochea maendeleo ya Watanzania.
Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Kigoma Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyewakilishwa na Dkt. Rashid Chuachua Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, ambaye alisema kuwa kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kunakofanywa na TRA kumesaidia Serikali kutekeleza miradi mikubwa kwenda kwa wananchi na kuwataka wafanyabiashara kutojihusisha na biashara za magendo kwani licha ya kuinyima mapato Serikali lakini pia inasababisha kuingiza bidhaa ambazo hazina viwango na hatari kwa afya.
Dkt. Chuachua alisema kuwa Serikali ya Mkoa wa Kigoma inaipongeza Mamlaka ya TRA mkoa wa Kigoma kwa kazi kubwa ya kukusanya kodi na kufikia malengo ya ukusanyaji yaliyowekwa jambo ambalo linaifanya serikali kuweka mazingira wezeshi ya kuifanya Mamlaka hiyo kutimiza malengo yake kwa ufanisi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.