ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 30, 2024

MBUNGE MTEMVU AFANYA KWELI ASHUSHA NEEMA UJENZI WA ZAHANATI GOGONI

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAMBA 

Mbunge wa Jimbo la Kibamba Issa Mtemvu ameingilia kati na  kumaliza sakata la mvutano na mgogoro wa mradi wa ujenzi wa zahanati katika mtaa wa gogoni kata ya Kibamba ambao umedumu kwa pindi kirefu bila ya kuanza kujengwa.

Kukwama kwa mradi huo umeleta hali ya sintofahamu kwa wananchi,viongozi wa serikali,na wa chama cha mapinduzi  kutokana na kusuasua kwa kwa kipindi cha muda mrefu  licha ya kuwepo kwa eneo lililotolewa na serikali.



Kutokana na hali hiyo imemlazimu  Mhe.Mtemvu kuamua kufanya ziara yake ya kikazi   yenye lengo la kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo  inayoendelea  kutekelezwa  na ile iliyokwama ili kuweza kuitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Mtemvu alibainisha kwamba lengo la Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuboresha huduma ya afya ili wananchi waweze kuondokana na changamoto za matibabu.

"Nipo katika ziara yangu ya kikazi lakini lengo lake kubwa ni kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ambayo imekwama na ile ambayo inaendelea kutekelezwa,"alibainisha Mhe.Mtemvu.

Aliwaomba viongozi wa chama na serikali kukaa kwa pamoja na kuondoa kabisa tofauti zao kati ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Gogoni pamoja na diwani wa kata ya Kibamba na atopenda kuona mradi huo unakwama tena na badala yake umalizike.


Katika hatua nyingine aliwaomba viongozi wa chama pamoja na serikali kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwa sambamba na kuhudhuria vikao vya maamuzi ya pamoja ili kuondoa hali ya  kuwepo kwa vikwazo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Gogoni Ally Mohamed alisema wananchi walipatiwa eneo hilo na serikali kwa lengo la mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ili kuwasaidia wananchi kupata huduma.

Naye Diwani wa Kata ya Kibamba Peter Kilango amesema kwamba hapo awali kulikuwepo na  changamoto kutokana na kutokubaliana na baadhi ya viongozi lakini ujio wa Mbunge umeweza kuwa mkombozi ya kuliweka sawa jambo hilo.

Katika hatua nyingine Mbunge Mtemvu ametembelea miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara ambapo amejionea ujenzi wa Makalavati mapya na madaraja  katika kata za Kwembe na Msigani.

Nao baadhi ya wananchi wamepongeza juhudi za Mbunge huyo katika kuleta chachu ya maendeleo na kumuomba aongeze nguvu katika kuwasaidia kumaliza changamoto ya maji na miundombinu ya barabara kwa baadhi ya maeneo.

Mbunge wa Jimbo la Kibamba Mhe.Issa Mtemvu amefanya ziara yake ya kikazi katika kata tatu za Kibamba,Kwembe,na Msigani ambapo amekagua miradi na kusikiliza kero na changamoto za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.