ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 12, 2025

WAZIRI ULEGA "SITOONGEZA HATA SEKUNDE UJENZI BARABARA NA DARAJA LA MKUYUNI" - MKANDARASI ATOBOA SIRI

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Mnamo Disemba 5, mwaka huu 2025 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt, Mwigulu Nchemba alifanya ziara jijiji Mwanza kuzitembelea familia zilizopata madhara ya vurugu za uchaguzi Mkuu wa Oct 29/2025. Pamoja na kuzungumza na wakazi wa jiji hili la miamba, pia Waziri Mkuu alipokea kero sugu ya kutokamilika kwa barabara na madaraja kadhaa likiwemo lile la eneo muhimu la Mkuyuni. Katika sehemu ya majibu yake Mhe. Waziri mkuu alitoa agizo kwa Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdalah Ulega kuja na kulikagua daraja hilo haraka iwezekanavyo na kutoka na suluhisho. Mwanahabari wetu Albert G. Sengo anakuja hapa na taarifa kamili. Lakini kwanza hebu tujikumbushe kauli ya Waziri Mkuu aliyoitoa mnamo Disemba 5 2025.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment