Moto huo umeunguza baadhi ya mashine mpya za kiwanda hicho sambamba na makasha mengi yaliyokuwa yakisubiri kupelekwa viwanda vingine vilivyopo jijini Mwanza, Mara na Kagera kupakiwa minofu ya samaki kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.
Wafanyakazi wa kiwanda hicho waliozungumza na mwandishi wa habari waliofika katika tukio hilo kwa sharti la kusitiriwa majina yao wamesema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme kwa mitambo iliyosababisha cheche za moto zilizoruka hadi kwenye makasha ya maboya ambayo tayari yalikuwa yamezalishwa.
Mashuhuda hao wameongeza kuwa kuwa moto huo baada ya kudaka maboya ulishika kasi na kunasa katika sehemu nyinginezo kiwandani hapo zikiwemo mashine na vifaa vingine kabla ya kikosi cha zima moto kufika na kuudhibiti moto huo.
Biju Zacharia (wa3 kutoka kulia) ambaye ni meneja uzalishaji wa kiwanda hicho amesema kuwa bidhaa nyingi zizalishwazo kiwandani hapo zimeungua na pia moto huo uleta hasara kubwa ambayo bado haijafahamika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.