Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua mgodi wa kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) kabla ya kuzungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua baadhi ya maeneo ya uzalishaji madini ya dhababu kwenye kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Na Mathias Canal, Lindi
Kamishna msaidizi wa madini kanda ya kusini Ndg Mayigi
Makorobela ameagizwa kuanzisha haraka ofisi ya Madini Wilayani Ruangwa ikiwemo
kupeleka wataalamu ili kurahisisha huduma za kitaalamu kwa wachimbaji wadogo
ikiwemo elimu ya usalama kazini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametoa
agizo hilo leo tarehe 18 Januari 2018 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo
waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya
Megembekenyela wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.
Alisema kuwa Wizara ya Madini imeamua kuanzisha ofisi hiyo
kutokana na maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Kassim Majaliwa aliyoyatoa hivi karibuni wakati alipokuwa ziarani Mkoani humo
ambapo alibaini kuwa wachimbaji wadogo wanapata kadhia kubwa kutokana na umbali
wa ofisi kwani wanalazimika kutumia zaidi ya kilomita 45 kuzifikia ofisi za
madini zilizopo Wilayani Nachingwea.
Alisema kuwa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa anawapenda
wachimbaji wadogo nchini ambao hata hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu
alibainisha kukusudia kuwanufanisha watanzania kupitia rasilimali zao ikiwemo
madini.
"Mhe Rais Magufuli anataka wananchi wote wanaoishi karibu na
mgodi kunufaika na rasilimali zao, nyote mtakuwa mashahidi, tangu nchi
iliporuhusu uchimbaji wa madini hakuna manufaa ya moja kwa moja kwa watanzania
badala yake madini yamekuwa yakinufaisha mataifa mengine ambayo baadaye
tunayapigia magoti kuyaomba msaada" Alikaririwa Mhe Biteko huku akipigiwa
makofi na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo
Mhe Biteko alisema kuwa lengo la kuanzisha ofisi ya madini
katika Wilayani hiyo ya Ruangwa ni kuwarahisishia wachimbaji kuwa na jukumu
moja la kuchimba na kuuza rasilimali wanazozipata kwani watakuwa sehemu ya
kuchagiza maendeleo sambamba na kuinufaisha serikali kutokana na ulipaji kodi.
Aliwasihi wachimbaji hao kuendelea kuunga mkono juhudi za
serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwani tangu
ameingia madarakani katika kipindi kifupi ameimarisha nidhamu mpya kwa kila
mtanzania na usimamizi madhubuti wa rasilimali za Taifa.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka
Biteko ameipongeza kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini
Exploration & Mining Services (GEMS) ambayo ni kampuni ya wazawa kwa
kufanya kazi kwa kufuata vyema sheria na taratibu za uchimbaji.
Alisema kuwa kampuni zingine zinapaswa kujifunza kwa kampuni
hiyo ya GEMS kutokana kulipa kodi mbalimbali kwa uwazi na ushiriki wa shughuli
mbalimbali za kijamii ikiwemo kusaidia sekta ya afya, Maji, sekta ya elimu
sambamba na michezo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.