ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 27, 2018

MTOTO WA RAIS WA ZAMANI WA ANGOLA AZUIWA KUONDOKA NCHINI KWA TUHUMA ZA UFISADI.

Mtoto wa rais wa zamani wa Angola azuiwa kuondoka nchini kwa tuhuma za ufisadi
Mtoto wa kiume wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos amezuiwa kuondoka nchini kutokana na tuhuma za ufisadi zinazomuandama.
José Filomeno dos Santos anatuhumiwa kuhamisha kiasi cha dola milioni 500 za Marekani kutoka hazina ya taifa aliyokuwa akiiongoza, hadi kwenye akaunti binafsi.
Duru za habari zinasema, mtoto huyo wa rais wa zamani wa Angola alihamisha fedha hizo kutoka Benki Kuu ya Taifa hadi kwenye akaunti ya Benki ya Credit Suisse iliyoko nchini Uingereza.
Luís Benza Zanga, Mwanasheria Mkuu wa Angola jana Jumatatu aliwaambia waandishi wa habari mjini Luanda kuwa, chama tawala cha MPLA kilihusika pakubwa katika ubadhirifu huo mkubwa wa fedha za umma.
Amesema Valter Filipe, aliyekuwa Rais wa Benki Kuu ya nchi hiyo pia anachunguzwa katika kashfa hiyo ya ufisadi wa kiuchumi.Angola, moja ya wazalishaji wakubwa wa mafuta inakabiliwa na tuhuma za ufisadi

Rais wa sasa wa Angola, João Lourenço  Januari mwaka huu alimfuta kazi mtoto huyo wa kiume wa mtangulizi wake, kuwa mkuu wa hazina hiyo ya kistratajia ya serikali yenye zaidi ya dola bilioni 5.
Nafasi hiyo ilijazwa na Carlos Alberto Lopes, Waziri wa Fedha wa zamani wa nchi hiyo.
CHANZO/Parstoday swahili

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.