ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 30, 2018

HATIAMAYE BOMBARDIER YA TANZANIA ILIYOZUILIWA NCHINI CANADA YAACHILIWA.

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewathibitishia wananchi kuwa ndege yake aina Bombardier Q400 iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada imearuhusiwa kuondoka nchini humo na muda wowote kutoka sasa itawasili hapa Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa leo Machi 30, 2018 kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akiweka picha zilizokuwa zikionesha ndege hiyo wakati wa matengenezo ya mwisho kabla ya kuruhusiwa kuondoka.

“Ndege yetu aina ya Bombardier Q400, iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada ilikwishaondoka Canada kuja Tanzania. Pia ndege kubwa nyingine tatu (2 Bombardier CS300 kutoka Canada na  1 Boeing 787-8 Dreamliner) kutoka Marekani, zitawasili baadaye mwaka huu. Nawatakia Ijumaa Kuu njema”, amesema Msigwa.

Aidha, Msigwa amesema hawajajua tarehe maalumu ya kutua ndege hiyo katika ardhi ya Tanzania kutokana na baadhi ya vitu kuwa vinamaliziwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.