ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 14, 2019

IJANA WA UMRI CHINI YA MIAKA 25 HATARINI KUAMBUKIZWA VVUxMWANZA

 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Emil Kasigara akizindua rasmi Jukwaa la “SITETELEKI” litakalozungumzi maswala ya Afya hususani Vijana chini ya mika 25 ili waweze kujitambua na kuwa na tabia chanya. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

 Mtaalamu wa maswala ya Afya kutoka Wizara ya Afya, Gerald Kihwele akiwakilisha maada ya “SITETELEKI” kwa wadau wa Afya(hawapo pichani) litakalozungumzia maswala ya Afya kwa Vijana chini ya miaka 25 mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa hilouliofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.
 Wadau wa Afya kutoka sekta tofauti wakisiliza maada mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la “SITETELEKI” litakazungumzia maswala ya Afya haswa kwa Vijana chini ya miaka 25 uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza
 Wadau wa Afya kutoka sekta tofauti wakisiliza maada mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la “SITETELEKI” litakazungumzia maswala ya Afya haswa kwa Vijana chini ya miaka 25 uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza
Wadau wa Afya kutoka sekta tofauti wakisiliza maada mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la “SITETELEKI” litakazungumzia maswala ya Afya haswa kwa Vijana chini ya miaka 25 uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza



UWEZEKANO wa Vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kushindwa kutimiza ndoto zao za maisha ni mkubwa endapo hawatapata elimu sahihi ya afya ya uzazi na maambukizi ya Ukimwi (VVU) itakayowasaidia kufanya maamuzi sahihi kwa mstakabali wa maisha yao.

Kundi hilo liko kwenye hatari hiyo kutokana na kukabiliwa na changamoto za ongezeko la maambukizi mapya ya VVU na mimba za utotoni kwa sababu ya uelewa mdogo (elimu) na upungufu wa huduma rafiki za afya ya uzazi na VVU kwa vijana.

Akizindua Jukwaa la Vijana ( SITETEREKI  Najifunza Kila Hatua ) kaimu Katibu Tawala wa msaidizi Mkoa wa Mwanza Emily Kasigara alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya wakishirikiana na Mradi wa USAIDI Tulonge Afya i 360 imeanzisha jukwaa hilo  la vijana ili kuwajengea uwezo katika masuala ya afya ya uzazi na Ukimwi, wajitambue na kubadilisha tabia zao.

Alisema serikali, jamii na wadau wana kazi kubwa ya kuwaelimisha vijana kujitambua , wakijitambua na kujali afya zao kutakuwa na matokeo chanya kwao na watafanya maamuzi sahihi, hawatachezea afya zao na kuwahimiza waende vituo vya huduma za uzazi na kupima afya. “Jukwaa la SITETEREKI Najifunza kila hatua  litakuwa kimbilio la vijana kufikia maisha wanayoyahitaji kwani ni eneo muhimu ambalo ni nguvu kazi na taifa la kesho, watapata mahali pa kutoa dukuduku zao na watajengewa uwezo.

Lengo la serikali wafikiwe ili wasijiingize kwenye changamoto 
zinazowaharibu na kuhatarisha maisha yao ya baadaye,”alisema Kasigara.

Alisema serikali imeanzisha jukwaa hilo litakalowawezesha kuwa na maisha bora baada ya kujengewa uwezo  na kujitambuawatatimiza azma ya serikali ya Tanzania ya uchumi wa kati wa viwanda kwani familia ikiwa duni kiafya haitakuwa na mchangokwenye uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Mratibu wa Elimu Afya ya Uzazi Wizara ya Afya  Dk. Gerald Kihwele alisema licha vijana kuwa tegemeo kiuchumi wanakabiliwa na changamoto nyingi ambapo vijana wa umri wa miaka 15 hadi 24 sawa na asilimia 40 wana maambukizi ya VVU, kati ya hao asilimia 70 ni wasichana na ndio wanaokabiliwa na hatari ya maambukizi mapya.

Alisema ni asilimia  41 tu ya vijana wa kiume wanaozingatia njia za afya ya uzazi na wanatumia kinga kwa usahihi wakati wakujamiiana huku wasichana wanaopata huduma hizo wakiwa ni asilimia 37 na ndio wenye changamoto kubwa hivyo wakijengewa uwezo watajitambua na kusimama kwenye misimimo thabiti.

  Dk. Kihwele alieleza kuwa serikali inafanya jitihada kubwa za kuweka mazingira bora ya huduma ya afya ya uzazi kwa vijana na kuwafanya wawe sehemu ya mipango yake, hivyo lazima kuwe na huduma za viwango vya  kuwavutia na kuchochea fikrazao waende kwenye maeneo ya kutolea huduma.“Upatikanaji wa huduma rafiki za afya ya uzazi kwa vijana badosi za kuridhisha ni asilimia 30 hivyo hatuwezi kuwavutia vijana waende kupata huduma hizo ambapo  serikali zifikie asilimia 80 na ipo haja mitizamo ya watoa huduma ivutie na kuhamasisha vijana wazichangamkie,”alisema Dk. Kihwele. 

Naye Mshauri Mwandamizi wa SBCC Shahada Kinyanga alisema vijana hupewa  taarifa zisizo sahihi na wanakosa motisha ya kufikia malengo yao kimaisha  hivyo jukwaa la SITETEREKI  litajibu changamoto zao na kuibua hisia za kufikia matarajio na mahitaji yao,litawaongezea ukweli kabla yakujiingiza kwenye uhusiano  na kufanya uamuzi sahihi.“Tunalenga maeneo yatakayonyesha mafaikio makubwa  katika kuboresha afya za vijana wa Kitanzania wa umri wa miaka 15 hadi 24hasa huduma za afya ya uzazi kabla ya ujauzito,upimaji wa VVU na tohara ya hiari kwa wanaume.

Baadaye tutahusisha vipaumbele vya jamii na kimaisha kwani takwimu zinaonyesha VVU na mimba za utotoni husababisha afya duni na vifo kwa vijana,” Kinyanga.Alisema jukwaa hilo ambalo lipo  chini ya Wizara ya Afya,ndani ya mradi wa  miaka mitano wa USAID Tulonge Afya wanalenga kuwafikia vijana 22,800 kwa mwezi kwa kuwatumia wahamasishaji 520  katika Kanda ya Ziwa  na Magharibi na kati ya wahamasishaji hao 270 ni wasichana. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.