ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 5, 2012

MWANZA YAONGOZA KWA USAFI MWAKA WA 7

Tuzo zilizotangulia ofisi za jiji la Mwanza
Jiji la Mwanza kwa mwaka wa saba mfululizo limefanikiwa kuibukamshindi wa kwanza kwa usafi wa mazingira na zfya katika majiji nchini.

Awali Taarifa za matokeo zilitolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kuweendea makatibu Tawala wa mkoa iliyoshiriki ambapo hatimaye leo kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira mjini Kilimanjaro, Mwanza imekabidhiwa rasmi Kombe lake la ushindi wa kwanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Wilson Kabwe.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Bw. Wilson Kabwe ameeleza kufurahishwa kwake na rekodi hiyo ya  ushindi mfululizo akiwataka wafanyakazi wa kitengo cha usafi pamoja wanasiasa, wauguzi wa afya na wananchi kwa ujumla kutobweteka na ushindi huo bali kuiunga mkono kwa dhati kampeni hiyo ili kuhakikisha jiji linakuwa safi muda wote.

Majiji ya Tanzania yaliyoshindanishwa kwenye mchakato huo ni pamoja na jiji la Dar es salaam, Tanga, Arusha na Mbeya
Kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makamau wa Rais mh. Charles Kitwanga akipata maelezo toka kwa Bi Arafa Maggid mhandisi mazingira Bonde la pangangi kuhusu vifaa vya kupimia ubora wa maji, alipotembelea banda la hilo leo katika maonyesho ya wiki ya mazingira mkoani Kilimanjaro.

Kauli mbiu ya siku ya mazingira 2012 ni Hifadhi Mazingira Jikite Kwenye Uwekezaji Endelevu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.