Akihutubia wafuasi wake katika mkutano wa kisiasa katika Kaunti ya Narok mnamo Jumamosi, Agosti 6, Ruto alitaniana na umati kuhusu wakati wa kuamka kwa shughuli hiyo.
Katika mazungumzo yao, umati ulimwambia Ruto kuwa utaamka saa kumi asubuhi ili kwenda kupiga kura lakini kiongozi huyo wa chama cha UDA akasema kuwa kwa kuamka saa tisa watakuwa wamechelewa.
Ruto aliendelea kuulizana na umati: "Ati saa ngapi? Saa kumi? Mimi naona muamke saa tisa. Mimi naona saa kumi mnaanza kuchelewa. Sindio?" Kwa mujibu wa Ruto, iwapo wafuasi wake wataamka mapema na kumpigia kura, watahakikisha kuwa anambwaga mpinzani wake mkuu Raila Odinga mapema.
Ruto ametupia vijembe Raila ambaye ni mgombea wa Azimio akisema kuwa tayari mikakati ipo ya kuhakikisha anaastafu kabisa kutoka kwa siasa.
Tumekubali ni saa tisa? Ndio tumalize hii kura. Kabla ya mzee wa kitendawili hajaamka kura imekwisha. Mnanisikia jameni? Na tayari tumemtayarishia wilibaro. Si mmeona wilibaro?" Ruto alisema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.