ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 3, 2022

MALIMA AKABIDHIWA OFISI RASMI.

 

🖐🏾Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu mpya wa Mkoa Mwanza, Adam Malima.


Akizungumza kwenye makabidhiano hayo yaliyofanyika leo Agosti 03, 2022, Mhandisi Gabriel amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuwezesha kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha kuanzia Juni 11, 2021 hadi Agosti 01, 2022.


Pia ametumia nafasi hiyo kuwaasa watumishi mkoani kutoa ushirikiano kwa Malima, kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kutojihusisha na rushwa pamoja na kumuombea Rais Samia ili Taifa lizidi kwenda mbele zaidi kimaendeleo.


"Lipendeni Taifa lenu la Tanzania kwani watumishi mmepewa dhamana katika nafasi mbalimbali hivyo mnapaswa kutumia akili zenu na elimu mliyonayo ili kuweza kulitendea haki Taifa, ukiendekeza rushwa unalisaliti Taifa lako" amesema Mhandisi Gabriel.


Kwa upande wake Mkuu mpya wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima ameahidi kushirikiana vyema na watumishi mkoani Mwanza ili kuendeleza utendaji kazi wenye tija kimaendeleo.


Amesema Mwanza ni Mkoa wa kimkakati kiuzalishaji na biashara hivyo atashirikiana na wafanyakazi na wafanyabiashara katika sekta za umma na binafsi ili kupata mawazo yao yatakayokuza maendeleo ya Mkoa.

.

.

#DriveMix

@mcsuzuki_

@gsengoTv

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.