Waziri wa maji Juma Aweso akiwa na viongozi wa wilaya ya Iringa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika kata ya Masaka Mkoani Iringa.
Waziri wa maji Juma Aweso akiwa mkuu wa wilaya na viongozi wengine wilaya ya Iringa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika kata ya Masaka Mkoani Iringa.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza waziri wa maji Juma Aweso akiwa mkuu wa wilaya na viongozi wengine wilaya ya Iringa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika kata ya Masaka Mkoani Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
WAZIRI
wa maji Juma Aweso amewapongeza uongozi wa wilaya ya Iringa kwa kusimamia
vizuri ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika bodi ya maji bonde la
Rufiji kwa kuwa litafanikisha kuleta maendeleo kwa wananchi na kutatua
changamoto ya maji kwa wananchi wa kata ya Masaka.
Akiwa
katika ziara ya kiazi mkoa wa Iringa waziri Aweso alisema kuwa ameridhishwa na
ujenzi wa mradi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kijiji cha Sadan kwa
kuwa mmoja ya miradi mingi mikubwa ambayo itakuja kuwa na matokeo ya moja kwa
moja kwa wananchi wanaolizunguka bwawa hilo.
Aweso
alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeigiza wizara ya maji
kuhakikisha inachimba mabwawa ya kila wilaya ili kutatua changamoto hiyo na
kuongeza njia za kukuza uchumi wa maeneo husika.
Alisema
kuwa kukamilika kwa bwawa hilo kutaisaidia kuleta maendeleo ya miradi mingine
ya maji kutokana na usimamizi mzuri ambao unafanywa na uongozi wa wilaya na
mkoa kwa ujumla kwenye maendeleo ya miradi ya kijamii.
Alisema
mradi huo wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua utagharimu kiasi
kikubwa cha fedha ambacho ni 900,982,000/= ambazo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu
Hassan amezileta kutatua changamoto hizo kwa wananchi wa kata ya Masaka.
Akijibu
maombi ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephen Mhapa na diwani
wa Masaka Methew Nganyagwa alisema kuwa wanayafanyia kazi maombi yao na tayari
suala la kuchimba bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kijiji cha Magubike
lipo kwenye mpango wa fedha za mwaka huu na ombi la matank ya maji wataletewa
mapema iwezekavyo.
Awali
akisoma taarifa ya mradi kwa waziri,msimamizi wa mradi huo Eng Geofrey Simkonda
alisema kuwa mradi wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua ni mkakati wa
uendelezaji,utumiaji,uhifadhi na usimamizi wa vyanzo vya maji katika bonde la
Rufiji.
Alisema
kuwa lengo la ujenzi wa mradi huo wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua
ni kuvunia maji na kurahisiha upatikanaji wa maji kwa wananchi hususani wenye
uhaba wa rasilimali za maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kibinadamu.
Eng
Simkonda alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Iringa,kata ya Masaka inayojumuisha
Vijiji vya Makota, Sadan na Kaning'ombe watanufaika na mradi huo.
Alisema
kuwa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua la Masaka lina kimo cha mita 14,urefu
mita 260 na litakuwa na ujazo wa mita 439,803 na ujenzi unatarajiwa kukamilika
mwezi wa tisa mwaka 2022 hadi sasa mradi umefikia asilimia 50.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa
anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa
utatua kero za wananchi pamoja na kuleta maendeleo kwa wananchi.
Alisema
kuwa kukamilika kwa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kijiji
cha Sadan kutachochea maendeleo ya wananchi kiuchumi kwa shughuli ambazo
zitakuwa zinafanywa katika eneo hilo.
Naye
diwani wa kata ya Masaka Methew Nganyagwa alisema kuwa mradi huo utawanufaisha
zaidi ya wananchi 7000 kwa shughuli mbalimbali za wananchi ambazo watakuwa
wanazifanya kwenye mradi huo wa bwawa.
Nganyagwa
alisema kukamilika kwa bwawa hilo licha ya kuondisha changamoto ya miaka mingi
ya ukosefu wa maji Safi na salama, pia kutafungua na kuchochea fursa ya ukuaji
wa kiuchumi kupitia fursa ya Kilimo cha umwagiliaji, Uhakika wa maji kwa ajili
ya mifugo pamoja na shughuli za uvuvi na biashara ya samaki katika Vijiji
vinavyozunguka kata hiyo.
Nganyagwa akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa kata ya Masaka alisema Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kwa vitendo dhamira ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kuwakumbuka wakina mama na wananchi masikini waliopo vijijini kwa kuwasogezea miradi mbalimbali hivyo ahadi ya wananchi ni kuendelea kumuunga mkono na kumuombea ili kufanikisha malengo ya maendeleo kupitia Serikali yake ya awamu ya sita.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.