Mapenzi ni kitu cha ajabu sana, watu kutoka koo, makabila, mataifa na wenye rangi tofauti hujikuta katika dimbwi zito. Hujikuta katika wakati ambao kila mmoja haoni kitu kingine cha thamani zaidi ya mpenzi wake. Huu ni wakati ambao si tu kuwa neno usaliti linakuwa halipo bali wapenzi hawahisi hata kama kuna maisha bila ya yule wampendaye.
Usaliti ni jambo lenye maumivu yasiyovumilika hasa ikiwa ni jambo ambalo halikutarajiwa. Mtu hahisi kama itatokea mpaka inapotokea. Mwishoni mwa wiki hii kumeenea picha za mwanaume aliyejikatisha uhai kisa mapenzi. Hii ikanikumbusha utafiti usio rasmi nilio ahi kufanya juu ya kwanini wanaume huumizwa zaidi na usaliti kuliko wanawake.
Sababu 4 za kwa nini wanaume huumia zaidi kwenye mapenzi
1. Wanaume si wepesi kusema yaliyowasibu.
Ukisikiliza vyombo vya habari au kusoma magazeti ni rahisi kukuta story ya mwanamke anayelalama baada ya mpenzi, mchumba au mume au mume kutoka na mwanamke mwingine. Lakini ni nadra sana kukuta mwanaume akilalama! Si kwa kuwa hawaumizwi au hawana majeraha, bali ni sababu kwa wanaume inaonekana kama kujidhalilisha kusema hivyo.
Hawatamani hata rafiki zao. Huishia kuumia peke yao, huishia kuhuzunika peke yao hiyo hupelekea kujenga majeraha makubwa moyoni. Kuendelea kufuga hasira ambazo saa nyingine hupelekea wao kufanya maamuzi ya ajabu na yenye kustaajabisha kwa jamii.
2. Mwanaume hupenda kuendelea kuwa na nguvu juu ya jambo fulani siku zote
Ndiyo, kwa mwanaume kuwa na watu wanaomtii, wenye kumheshimu na kumsikiliza ni jambo linalompa faraja na kumfanya ajivunie. Mwanaume anapokuwa na mwanamke hupenda kuona huyo mwanamke akimnyenyekea, akimtii na kumsikiliza, Kwa taarifa yako mwanaume hapendi hata yule mwanamke asiyempenda awe wa kwanza kusema imetosha,au awe na mwanaume mwingine, inapotokea hayo humfanya mwanaume ajione amepungikiwa kitu, humfanya ahisi yeye si bora tena hapo ndipo tatizo linapoanzia.
3. Wanaume wana tabia ya kumuamini sana mwanamke wanayekuwa naye
Moja kati ya kazi ngumu kwa mwanamme ni kumfanya amwamini mtu mwingine kwa kiwango kikubwa, Inaweza kuchukua miaka mpaka kufikia hatua ya kumuamini mtu mwingine hasa mwanamke. Lakini inapotokea akafanya hivyo huamini jumla. Hatua ya kumuamini sana mwenza wake huleta madhara makubwa mbele ya safari.
Tofauti na mwanamke ambaye siku zote anakuwa anawasha taa ya tahadhari na kujua inawezekana saa yoyote mpenzi wake atachepuka na inapotokea kweli mshtuko wake hauwezi kuwa sawa na mwanaume ambaye humwamini sana mwenza wake. Mwanamke anaweza kuzama kimapenzi au hata kuolewa na mwanaume asiye mwamini ni ngumu kwa mwanaume kufanya hivyo.
4. Sio rahisi kwa mwanaume kuhamisha upendo
Katika ulimwengu wanaume ndiyo wanaongoza kwa kuwa wasaliti kuna msemo unasema ‘every guy cheats’, ukweli tusioujua ni kuwa pamoja na kuwa wanaume hucheat zaidi kuliko wanawake ila wanafanya hivyo kwa sababu ya tamaa ya miili na nafsi zao hubaki kwa wenza wao wa kudumu
Si rahisi kwa mwanaume kumuacha mwanamke anayempenda na kuhamishia mapenzi hayo kwa mwanamke mwingine. Mwanamke anapokuwa mpweke Nna akatokea mtu ambaye akamtolea ule upweke anakuwa ameuwin moyo wake.
Usaliti umetokea ameamua alivyoamua, huo sio mwisho wa maisha kuna sababu nyingi za wewe kuendelea kuishi na kufurahia maisha. Pengine haya yanaweza kusaidia kukuamsha tena na kuona maisha yapo na hakuna sababu ya wewe kuumia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.