Moja kati ya matukio ya kusisimua ni ushirikiano alio nao Mh. Luhaga na vyama vingine ambapo Mwenyekiti huyu wa moja ya vijiji jimboni humo kupitia chama cha CHADEMA Sita Ngeniobuyu alijumuika kusikiliza shukurani za Mbunge wake na hakusita kumshika mkono kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Wilaya ya Meatu, Mkoa mpya wa Simiyu Mh. Luhaga Joelson Mpina akitunzwa kiasili na akinamama kupitia mila za kabila la Wasukuma jimboni humu.
Ujenzi wa barabara pamoja na madaraja ni moja ya changamoto kubwa za maendeleo Jimboni Kisesa.
Tangu kipindi cha Uchaguzi 2005 Jumla ya madaraja sita yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 yamejengwa yakipitika ambayo ni pamoja na daraja la mto Simiyu, Tingabuligi, Sakasaka, Lingeka, Lubiga na Longalonhiga.
Zaidi ya bilioni 1.6 zimetengwa kupitia bajeti ya serikali kuipatia umeme wilaya ya Meatu na vijiji vyake ambapo mpaka sasa miundombinu ya nguzo imekwisha simikwa huku mradi ukitegemewa kukamilika rasmi mwezi desemba 2011.
Sehemu ya wakazi wa Jimbo la Kisesa waliofurika kumlaki mbunge wao.
Akiwa kama moja ya waalikwa meza kuu kwenye kusanyiko hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Lubiga kupitia CHADEMA Sita Ngeniobuyu alipata fursa ya kutoa shukurani zake kwa wananchi waliofurika kusikiliza shukurani na mipango ya maendeleo ya baadaye jimboni humo zake Mh. Mbunge Luhaga Joelson Mpina, pembeni yake ni Afisa Mahusiano Ofisi ya Mbunge Tito Paul Masele.
"Shauri zenu! jimboni humu sisi hatujali.. wewe ni wamashariki au magharibi tunapiga kazi pamoja kwani ni waajiriwa wa wananchi" Kauli ya katibu wa CCM wilaya ya Maswa Omary Kalolo (kushoto) aliyekuwa kivutio kwenye mkutano huo.
Wazee wa kijiji cha Mbugayabanyha wakimsikiliza kwa makini mbunge wao.
Kwa ajili ya kukuza michezo hapa Mratibu wa Elimu kata ya Lubiga bw. Emanuel Manyama akikabidhiwa vifaa vya michezo kwa kata yake.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mbugayabanyha bw. Charles akikabidhiwa vifaa vya michezo kwaajili ya kijiji chake.
Ili kudumisha mahusiano na afya vilevile kukuza michezo nchini naye timu manager wa Lubiga Shooting bw. Misomung'ombe naye alikabidhiwa vifaa vya michezo ndani ya kusanyiko hilo.
Tupe maoni yako
wabunge wa majimbo mengine igeni mfano wa Mh Mpina.ndani ya mwaka kashajenga madaraja 6 na kuweka nguzo za umeme na miradi mingine je, ikifika miaka 3 atajuwa wapi?Hongera sana Mh Mpina
ReplyDelete