Mchezo ulianza kwa kasi ya ajabu pasi za nguvu, wachezaji wa timu zote wakionana mithili ya game za soka barani Uropa na haikuchukuwa muda ilikuwa ni dakika ya 8 tu kipindi cha kwanza mchezaji Felix Sunzu aliwanyanyuwa mashabiki wa timu ya wekundu wamsimbazi kwa kupachika bao la kuongoza.
Toto wakicheza nyumbani wakiwa na kibri cha kuwa na mashabiki lukuki huku wakionana walifanikiwa kuichanganya ngome ya simba kwa samba la hatari likiongozwa na vifaa vipya walivyosajili mwaka huu hali iliyopelekea ngome yake kupoteza mwelekeo hivyo kusababisha madhambi na Toto kuzawadiwa penati, bila ajizi mshambuliaji wa kimataifa aliyesajiliwa na timu hiyo Darlington Enyina aliutumbukiza kimiyani mpira huo kuandika bao la kusawazisha ikiwa ni dakika ya 15 ya mchezo.
Toto ilijipatia bao la pili dakika ya 26 kupitia Mohamed Sudi , Simba ikasawazisha dakika ya 59 mfungaji akiwa Felix Sunzu.
Bao la tatu la Toto lilipatikana katika dakika ya 65 kupitia Iddi Mudy nao Simba kusawazisha tena bao hilo dakika tatu baadaye kwa mkwaju wa kiufundi wake mshambuliaji mahiri wa wanamsimbazi Patrick Mafisango.
Mchezo uligeuka kuwa wa upande mmoja kwa Simba kulisakama kama nyuki lango la Wanakishamapanda waliopoteza uelekeo mara baada ya moja kati ya kifaa chake Filemon mwendafile kulimwa kadi nyekundu akimkanyaga mgongoni tena kwa maksudi mchezaji wa Simba Kago.
Hadi mwisho ngoma droo Simba 3, Toto 3.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.