ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 22, 2011

MATUKIO KATIKA PICHA SIMBA NA TOTO AFRICANS

Toto na Simba jumatano ya tarehe 21sept2011 CCM Kirumba Mwanza.

Wachezaji wa timu ya Toto Africans wakipongezana kwa moja ya magoli yao yaliyopatikana jana.

Toto v/s Simba.

Mchezo huo ulishuhudia matukio kadhaa katika dakika ya 15 mashabiki walivunja geti la uwanja na kuingia uwanjani, lakini polisi waliweza kuthibiti tukio hilo kabla ya mbwa wa polisi kumponyoka askari na kuingia uwanjani na kuanza kukimbiza wachezaji ambapo alimfukuza zaidi Haruna Moshi na kusababisha mpira kusimama kwa dakika tano katika dakika ya 29.

Mbwa mwenye mfunzo akitweta mara baada ya saka-saka za kumfukuza Boban (hayupo pichani)aliyetimka kwa spidi kama farasi kushindikana kukamatika.


Nje nako:- mguu hapa, mbwa hapa. Usimamizi mbovu wa ukataji tiketi kwani kulikuwa na Hiace moja tu iliyokuwa ikikatisha tiketi kiasi cha kusababisha baadhi ya wapenzi wa soka kuchelewa kuingia na wengine kuahirisha kabisa kutinga dimbani humo.

Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la tatu la kusawazisha lililofungwa nae Patrick Mafisango katika dakika ya 69.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.