Mikoa ambayo amefanya utafiti ni pamoja na Mara, Pwani, Dar es salaam, Shinyanga, Mbeya, Manyara, Singida, Morogoro, Mtwara, Arusha, Tabora na Tanga pia katika mikoa hiyo kwa kipindi cha kati ya mwaka 2009 na 2011 zimefanyika jumla ya chaguzi ndogo za viongozi wa vijiji 84, mitaa 22 na vitongoji 248.
Kwa mujibu wa Nape, kati ya viti 84 vya wenyeviti wa vijiji, CCM kimefanikiwa kunyakua viti 83 sawa na asilimia 98.8, kati ya mitaa 22, CCM kimeshinda viti 17 sawa na asilimia 77.3 na kati ya vitongoji 248, CCM kimeshinda vitongoji 186 sawa na asilimia 75.
Akizungumzia kuhusu ukali wa maisha Mh. Nape anasema suala hilo linahusiana na uchumi wa dunia na si kwa nchi ya Tanzania.
Akizungumzia hatua ya aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kuachia nyadhifa zake za ubunge na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) akidai kuchoshwa na siasa uchwara lakini akarejea tena katika ulingo wa siasa kumnadi mgombea wa chama hicho Dk. Peter Kafumu, Nape amejitetea kwa kutoa mfano kwa kusema kuwa hata kanisani mtu akifanya kosa kuna adhabu maalum zilizo wekwa kama vile kutokushiriki meza ya bwana na kadhalika lakini siyo kwamba mtu huyo atakatazwa kuingia kanisani, ataingia kanisani kwa minajili ya kulishwa neno kuendana na utaratibu.
Amebainisha kubainisha kwamba Chama Cha Mapinduzi kinao mtaji wa wanachama ambapo katika kura za maoni kuwapata wagombea katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mgombea wa CCM alichaguliwa na wanachama 588 ilhali mgombea wa CHADEMA alichaguliwa wanachama 63.
Kupitia takwimu hizo Nape amejigamba kwa kusema kuwa CCM ina msingi mzuri iliyoujenga wa kushinda katika uchaguzi huo mdogo wa ubunge katika Jimbo la Igunga licha ya fitna zinazojitokeza kila kukicha toka kwa wapinzani wake, hivyo watu wasishangae siku chama hicho kitakapotangazwa kuwa mshindi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.