Afisa wa polisi akichukuwa maelezo toka kwa mmiliki wa roli hilo Godfrey Mwangi mara baada ya dereva kulitelekeza gari hilo na kutoweka kusiko julikana.
lameck Mongi Afisa Mfawidhi usimamizi Uthibiti na Doria wa Uvuvi mkoa wa Mwanza "Ndani ya nyaraka zilizogushiwa zinaonyesha gari lina mzigo wa tani 20 lakini mara baada ya ukaguzi tumegundua ni zaidi ya tani 40"
Kutokana na rasilimali ya uvuvi serikali ya Tanzania inajipatia mrabaha kupitia kodi za usafirishaji zao la samaki wakavu na wabichi hivyo utoroshaji wa bidhaa hizo unapofnyika unaikosesha serikali mapato.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya shilingi bilioni 3.7 zimekusanywa na serikali kupitia zao la samaki kwa mkoa wa Mwanza pekee.
Dalali wa serikali Henry Susuma "Mzigo kama huu ni wa kuharibika hivyo mara baada ya mzigo kukamatwa tu mahakama hutoa oda ya kuuzwa na pesa kupelekwa mahakamani kama sehemu ya ushahidi, taratibu zimekwisha fanyika kujua thamani ya mzigo kinachofuata ni mali kupigwa mnada"
Juma Makongoro mkuu wa doria udhibiti uvuvi haramu Mkoa wa Mwanza."Kitengo changu kimejipanga vizuri kuhakikisha kuwa mbinu zote za wahalifu zinadhibitiwa lakini yote yanafanikiwa kwa msaada wa wananchi walio wazalendo wa taifa hili"
Wavuvi wakianika dagaa katika fukwe za kijiji cha Nyamikoma mkoani Mwanza.
Bohari za kuhifadhia dagaa eneo la Nyamikoma wilayani Magu mkoani Mwanza, awali bohari hizi zilitumika kuhifadhia zao la pamba lakini mara baada ya zao hilo kushuka zimegeuzwa matumizi.
Tupe maoni yako
Kilichonisikitisha sio mimi hao sio dagaa wa kawaida ila ni watoto wa sangara, sasa hizo tani 40 ziwani sangara zitabaki na kukua mpaka zifikie kila 150? Jamani hii ni hatari kweli yaani watu wanavua watoto wa sangara eti ni dagaa ? ndo maana tunakosa samaki !
ReplyDelete