ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 16, 2022

RAIS SAMIA ATOA SALAMU ZA PONGEZI KWA RAIS MTEULE WILLIAM RUTO KWA USHINDI.


 Rais wa Tanzania Samia Suluhu amempongeza Rais mteule William Ruto kwa ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa 2022. 

Rais Samia Suluhu Ampongeza William Ruto Baada ya Kutangazwa kuwa Rais Mteule. Picha: Samia Suluhu. Chanzo: Twitter Katika taarifa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii siku ya Jumanne, Agosti 16, Suluhu alimpongeza Ruto kwa ushindi wake na kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuwa rais mteule. 

Suluhu pia aliwasifu Wakenya kwa kudumisha amani wakati wa mchakat mzima wa uchaguzi na kuahidi kuendelea kufanya kazi na Kenya. "Ninapenda kuwapongeza kwa dhati wananchi wa Kenya kwa kushiriki uchaguzi wao mkuu kwa amani na utulivu, ambapo matokeo yake ni Dkt William Ruto kutangazwa kuwa Rais mteule wa Kenya.

Tanzania itaendeleza undugu na ushirikiano wa Kihistoria na Kenya uliodumu miaka na mikaka," alisema. 

Suluhu pia aliahidi kuendelea kufanya kazi na Kenya ili kueneza uhusiano wao kidiplomasia. Rais huyo alibainisha kuwa Kenya na Tanzania zina uhusiano wa kihistoria kama majirani, akiongeza kuwa mataifa hayo mawili yameungana. 

Ruto apokea kongole kote duniani Baada ya kutangazwa rais mteule, William Ruto amekuwa akipokea jumbe za kongole kutoka kwa viongozi tofauti ulimwenguni. 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alisema anaamini kuwa Ruto atahudumia Wakenya bila upendeleo. 

Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamed alisema anatazamia kufanya kazi na Ruto katika kuendeleza maslahi ya pande zote mbili za Nairobi na Mogadishu.

 Ubalozi wa Marekani ulitaja kuchaguliwa kwa Ruto kuwa rais wa tano kama hatua muhimu huku ukizitaka pande ambazo hazijaridhika na matokeo kupinga matokeo hayo kupitia mifumo iliyopo ya kutatua mizozo. Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alimtakia kila la heri Ruto akiahidi kufanya kazi naye kwa karibu ili kuboresha uhusiano baina ya nchi hizo mbili. 

PIA SOMA Magazetini Agosti 16: William Ruto Alizungumza na Raila Kabla ya Kutangazwa Rais Mteule Katika salamu zake za pongezi, rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema anatazamia uhusiano thabiti kati ya Nigeria na Kenya. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.