MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba katika akiongoza matembezi maalumu ya kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika nchini Agosti 23 mwaka huu kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Manyema na kushoto ni Mkuu wa wilaya Tanga Hashim Mgandiliwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillooo

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa akizungumza kuhusu namna walivyojipanga kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema Sensa ya watu na makazi ina umuhimu mkubwa sana kwa vijana kwa sababu wao ndio Taifa la leo na kesho hivyo mipango mingi inayopangwa inawagusa kwa sababu jambo hilo sio la kila mwaka bali ni kila baada ya miaka 10.
Mgumba aliyasema hayo leo wakati wa matembezi kwa ajili ya kuhamasisha zoezi Sensa ya Watu na Makazi iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga ambapo alisema sensa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Alisema kwa hiyo mipango ya miaka 10 ijayo itategemea idadi ya watu na makazi na shughuli zitakazobainika baada ya Sensa hiyo kukamilika hivyo ndio maana Rais Samia Suluhu ametoa siku hiyo kuwa ya mapumziko kutokana na umuhimu wake.
"Nimeamini Tanga hatuna dogo na jambo la mama ni letu wana Tanga mmedhihirisha kwa vitendo hili lililofnyika Tanga linafanyika na wilaya nyengine lengo ni kuhamasishana tujitokeze kwa wingi kushiriki kwenye katoka zoezi la sensa ya watu na makazi kwani ni muhimu kwa maendeleo yetu ua mkoa na Taifa na itatusaidia kupata takwimu sahihi shughuli za watu na kufahamu uchumi wa watu hivyo kusaidia serikali kupanga mpango wa maendeleo
Alisema wasipopata idadi kamili ya watu itakuwa ni vigumu kwa serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa watu wake na baadae wao watalalamika kwamba serikali inapendelea na inapeleka miradi mingi mikoa fulani kwa sababu kule ndio walijitokeza kwa wingi wakati huo.
Alisema suala la sensa halina mahusiano yoyote na imani za kidini,kijadi wala kimila bali ni kupanga maendeleo kwa watanzania hususani wakazi wa mkoa huo wa Tanga
Hata hivyo aliwataka wakazi wa mkoa huo kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23 mwaka huu hapa nchini
Awali akizungumza wakati wa matembezi hayo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alisema matembezi hayo yalikiwa ni muhimu kwa ajili ya uhamasishaji watu kujitokeza kwenye zoezi sensa ambapo wametembea umbali wa kilomita 7 kutoka kwenye viwanja vya urithi kuzunguka maeneo mbalimbali Jijini humo na kurejea walipoanzia.
Alisema wameanzisha mpango wa mtaa kwa mtaa Tanga na Sensa 2022 wana vijana 40 madensasi wanapita kila mtaa yote ya Tanga na kutoa burudani kwa dakika tano na kutoa ujumbe wa sensa anasma wanaamini kupitia mpango huo wanaweza kuwafikia watu wengi Jijini humo

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.