Mwanahabari Olivier Dubois mwenye umri wa miaka 48 kutoka Ufaranasa Jumanne amerejea nyumbani baada ya kushikiliwa kwa karibu miaka 7 kwenye eneo la Sahel.
Mwanahabari huyo alilakiwa na familia yake pamoja na rais Emmanuel Macron, kwenye uwanja mmoja wa ndege karibu na mji mkuu wa Paris.
Dubois
akiwa na mfanyakazi wa kutoa msaada Jeffery Woodke mwenye umri wa miaka 61
kutoka Marekani walikamatwa kusini magharini mwa Niger Okotoba 2016, na
waliwasili kwenye mji mkuu wa taifa hilo wa Niamey Jumatatu baada ya kuachiliwa
huru.
Video iliyotolewa awali na watu
waliokuwa wamemshikilia inasema kwamba walikuwa ni kutoka kundi la Support
Group for Islam and Muslims, GSIM, ambalo linajumuisha makundi ya kigaidi ya
Sahel, na linalohusishwa na lile la Al-Qaeda.
Dubois alikuwa akiishi nchini Mali
tangu 2015 wakati akiwa mwanahabari huru wa gazeti la Ufaransa la Liberation,
pale alipokamatwa. Hakuna taarifa za kina zilizotolewa kuhusu Dubois na mwenzake
Woodke.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.