ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 24, 2023

HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO KUANZISHA KLINIKI ZA KIBINGWA ZA JIONI

 

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhan


HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo inatarajia kuanzisha huduma za Kliniki za Kibingwa wakati wa muda wa ziada wa jioni itakayoanza kuanzia Aprili 9 mwaka huu katika hospitali hiyo.

Akizungumza leo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhan amesema huduma hizo zitaaza saa tisa na nusu jioni mpaka muda ambao wagonjwa watamalizika ambao watapata fursa ya kuonana na madaktari bingwa waliopo kwenye hospitali hiyo.

Dkt Juma alisema kwamba katika kliniki hiyo huduma mbalimbali za kibingwa ikiwemo magonjwa ya ndani,magonjwa ya ya upasuaji,magonjwa ya wakina mama,magonjwa ya watoto,magonjwa wa koo,pua pamoja na sikio .

Aidha alisema kwamba huduma hizo zitatolewa kwa wagonjwa wote wenye bima bila kujalia aina gani ya bima lakini pia wale wagonjwa wanaofanya malipo ya keshi yatapokelewa.

Hata hivyo alisema huduma hiyo itatolewa siku Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa tisa na nusu mpaka pale watakapomalizika.

Dkt Juma aliwahimiza wananchi wa mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kliniki hizo ili kuweza kukutana na madaktari bingwa wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga

Hata alisema uwepo wa kliniki hiyo utasaidia kutoa fursa kwa wagonjwa kuweza kukutana na madaktari bingwa ambao wataweza kuwasaidia hivyo watumie nafasi hiyo kuweza kuonana na madaktari hao bingwa waliopo kwenye hospitali hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.