ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 24, 2023

KIJANA ALIYEKWEPA KWENDA SHULE ILI AMTEMBELEE MPENZI AFARIKI KATIKA NYUMBA YA DEMU


Kijana aliyekwepa kwenda shuleni kwa lengo la kumtembelea mpenzi wake ameaga dunia katika nyumba ya binti huyo eneo la Northrise, mjini Ndola huko Zambia.

Emmanuel Kayuni mwenye umri wa miaka 21 anasemekana kuzirai na kuaga dunia katika nyumba ya mpenzi wake huku wazazi wake wakidhani kuwa alikuwa katiak shule ya bweni kule Mansa.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa eneo hilo Peacewell Mweamba, amesema tukio hilo lilitokea machi  22 ambapo plisi walipokea taarifa kutoka kwa baba wa marehemu, bwana John Kayuni

Taarifa fupi kuhusu suala hilo ni kwamba   marehemu alienda shuleni kule Mansa mwezi Januari 2023 lakini akatoka shule kukutana na mpenzi wake Princess Mwaba mwenye umri wa miaka 20,

Marehemu Emmanuel alikuwa amerejea kutoka shule ya bweni na kujificha kwa  mpenzi wake ili wazazi wake ambao waliamini kuwa alikuwa bado yuko shule wasijue.

Machi 21, 2023, marehemu na princess    walienda katika loji ya Executive kule Northrise ambako walilala na alikuwa anakilalamika kuhusu matatizo ya moyo.

Asubuhi, wawili hao walitoka loji na kwenda katika nyumba yao Princess ambako marehemu alimuacha demu wake mwendo wa saa tatu asubuhi ili aende gengeni kununua nyanya sokoni.

Saa moja baadaye, marehemu alizirai kwenye mlango alipokuwa akirejea kutoka kununua nyanya ambapo mfanyakazi wa kutunza maua na mashamba eneo hilo alimshuhudia akianguka.

Princess  alielezwa kilichotokea kwa Emmanuel na usafiri ukawasilishwa ili kumkimbiza hospitalini lakini akawa amefariki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.