Viongozi ya makundi ya walio wachache nchini India wanasema kwamba sheria mpya ya kutobadili Imani iliyopitishwa katika baadhi ya majimbo inalenga kuadhibu na kukandamiza makundi ya wakristo na waislamu nchini humo.
Hayo
yamejiri wakati tume ya Marekani ya Uhuru wa kimataifa wa dini, USCRIF,
ikieleza wasiwasi wake kutokana na sheria hiyo, na kuomba ibatilishwe.
USCRIF
kupitia ripoti imesema kwamba sheria hiyo mpya inavuruga uhuru wa kidini nchini
India, ambao tayari ulikuwa hatarini, na kwamba hatua hiyo ni kinyume na sheria
za kimataifa za haki za binadamu.
Makundi
ya kihindu pamoja na chama tawala cha Hindu Nationalist Bharatiya Janata,
wanadai kwamba wamishonari wa kikristo wanabadili Imani za watu kote nchini kwa
kutumia nguvu au ushawishi usiofaa.
Katika
miaka ya karibuni, wamedai kwamba waislamu wamekuwa wakivuta watu kwenye dini
yao kupitia njia haramu.
Kufikia
sasa majimbo 12 kati ya 28 yaliopo nchini humo yamepitisha sheria hiyo, wakati
baadhi ya yaliobaki yakitathimini kufuata nyayo .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.