Mwanamme mwenye umri wa miaka 37 anakabiliwa na mashataka ya mauaji baada ya mpenzi wake aliyefahamika kama Milca na mwenye umri wa miaka 48 kufariki wakati wakifanya ngono kichakani eneo bunge la Mbita kaunti ya Homa Bay.
Mtuhumiwa
anasemekana kumrithi marehemu baada ya kifo cha mume wake kama ilivyo tamadumi
ambapo mwanamke anaruhusiwa kurithiwa baada ya kifo cha mume wake
.Wawili
hawa wanasemekana kuwa walionekana wakibugia pombe katika kilabu kimoja eneo
hilo jioni ya kabla ya kuondoka kuelekea nyumbani.
Wakiwa
njiani hapo ndipo wasia wa kuyatia mahanjam katika mapenzi yao iliwajia na
kisha wakaamua kuingia kichakani eneo la Got Rateng na kushiriki tendo la ndoa
wasijuwe lilokuwa linawasubiri.
Mtuhumiwa
huyo aliyekutwa na kisa hicho amesemekana kuwa alijaribu kuuzika mwili wa
Milca.
Kulingana
na chifu wa Lambwe Mashariki Bernard Ouma wawili hawa walikuwa wameonywa dhidi
ya kubugia pombe na kuwa mshukiwa hakutarajia kuwa mpenzi wake angefariki
wakati wa ngono.
Amatuhumiwa
huyo alikamatwa baada ya kukiri kuwa marehemu alifariki wakati walipokuwa
wanashiriki ngono
Chifu wa
eneo hilo amesema kuwa alikuwa amefanya kikao na wawili hao awali na kuwaonya
dhidi ya hulka yao ya kufanya mapenzi kiholela baada ya kubugia vileo.
Mwili wa
mwendazake umepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Homa Bay uchunguzi zaidi
ukitarajiwa kufanywa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.