ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 21, 2023

MALAWI INAKABILIWA NA HATARI YA ONGEZEKO LA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU KUFUATIA UHARIBIFU ULIOSABABISHWA NA KIMBUNGA FREDDY AMBACHO KIMEHARIBU MIFUMO YA MAJI NA VYOO, WIZARA YA AFYA ILIONYA JUMATATU.



Nchi hiyo ambayo ilikuwa tayari ikipambana mlipuko mkubwa wa kipindupindu ambao haujawahi kurekodiwa wakati dhoruba ya kimbunga Freddy ilipotua wiki iliyopita, na kusababisha maporomoko ya matope na mafuriko, ambapo watu 476 walipoteza maisha na wengine takribani nusu milioni kukoseshwa makazi.

Mlipuko wa kipindupindu nchini humo uliozuka mwaka jana, ambapo watu zaidi ya 30,600 waliambukizwa na wengine zaidi ya 1,700 kupoteza maisha.


Baada ya mashambulizi ya kimbunga hicho kilichovunja rekodi, dhoruba hiyo ilisababisha vifo vya watu 579 katika nchi tatu za kusini mwa Afrika zikiwemo Msumbiji na Madagascar.

Malawi ni nchi iliyoathirika zaidi wakati kimpunga Freddy kiliposababisha mafuriko na maporomoko ya udongo ambayo yalisomba nyumba, barabara na madaraja – na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu ya maji nchini humo.



..................................................................................................................................................................................................................................................................................


WAKATI HUO HUO KUTOKA NCHINI MSUMBIJI


WAZIRI WA AFYA WA MSUMBIJI ALISEMA IJUMAA KUWA MLIPUKO WA KIPINDUPINDU KATIKA ENEO LILILOPIGWA NA KIMBUNGA FREDDY KIMEUA WATU WANANE WIKI HII NA WENGINE 250 WAMELAZWA HOSPITALI – IKIWA NI SEHEMU YA WATU 600 AMBAO NI WAGONJWA TANGU KUTUA KWA KIMBUNGA KATIKA ENEO HILO MWEZI FEBRUARI.

 

Waziri wa Afya Armindo Tiago amekiambia Radio Msumbiji inayomilikiwa na serikali kwamba waathirika wa kipindupindu walikuwa katika mji wa bandari wa Quelimane, mji mkuu wa Jimbo la Zambezia, eneo lililokuwa limeathiriwa sana na kimbunga hicho.

Tigao alisema hatua ya kuzuia kipindupindu imelengwa katika vituo 133 vya mji huo ambavyo vinatoa hifadhi kwa takriban watu 50,000 waliokoseshwa makazi kutokana na mafuriko. Ameongeza kuwa juhudi zaidi zinahitajika katika majimbo mengine yaliyokumbwa na Kimbunga Freddy, kimbunga cha historia ambacho kimepiga katika eneo hilo tangu Februari.

Tiago alisema kila mtu lazima afanye juhudi kudhibiti mlipuko huo kwa kuchemsha maji ya kunywa, kusafisha na kuosha chakula, na kutupa takataka inavyotakiwa – hususan choo cha binadamu. Iwapo watu wana dalili kama vile kuharisha na kutapika, lazima wafike katika vituo vya afya.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.