ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 21, 2023

POLISI WAMUUA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MASENO BAADA YA KUTUMIA RISASI KUWATAWANYA WAANDAMANAJI


Chuo kikuu cha Maseno kimempoteza mwanafunzi wa mwaka wa tatu William Mayange (pichani aliye chuchumaa) aliyekumbana na kifo chake baada ya polisi kutumia risasi kuwatawanya wanafunzi wa chuo hicho waliokuwa wakiandamana kulalamikia hali ngumu ya kiuchumi.

Mayange anasemekama kudhibitishwa kuwa amefariki alipofikishwa katika hospitali ya Coptic alikokuwa amepelekwa kupata huduma ya kwanza.


Marehemu  anasemekana kupigwa risasi shingoni alipokuwa amejumuika na wenzake nje mwa lango kuu la chuo hicho wakati wa maandamo yaliyokuwa yameitishwa na muungano wa Azimio ili kuishurutisha serikali kupunguza gharama ya maisha

Mayange alisoma katika shule ya upili ya Ringa Boys kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Maseno miaka mitatu iliyopita.

Polisi wamesema kuwa maandamano ya wanafunzi hao yalizua rapsha na kupelekea maafisa wa usalama kutumia risasi baada ya kuishiwa na vitoa machozi.

Maafisa wa usalama wamesema kuwa wanafunzi waliokuwa wakiandamana walionekana kuwashinda nguvu jambo ambalo lilichangia utumiaji wa risasi.

Maandamano ya Jumatatu 20 yameshuhudia makabiliano makali kati ya polisi wa wafuasi wa Azimio kote nchini.

 Kinara wa Azimio Raila Odinga ametangaza kuwa kila Jumatatu itakuwa ni siku ya maandamano hadi pale serikali itakaposhughulikia matakwa yao

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.