ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 25, 2023

"HAKUNA KURUDI NYUMA" RAILA AWEKA NGUMU, ASEMA MAANDAMANO YA JUMATATU YAKO PALE PALE.

 


Kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga amesema maandamano ya Jumatatu Machi 27 yataendelea kama yalivyopangwa. kiongozi wa ODM Raila Odinga alisema atakuwa kwenye maandamano. 

Akiongea eneo la Kisii ambapo alikuwa akihudhuria mazishi, Raila alisema kama serikali inataka asitishe maandamano lazima ifungue mitambo ya Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi. "Sisi haturudi nyuma, kama wanataka tusitishe wewe fungua servers. Kama unaamini ulishinda kwa nini unakataa kufungua servers," alisema Raila. 

Alizungumza wakati ambapo kuna presha kutoka kwa serikali na viongozi wa kanisa kuhusu maandamano. 

 Raila alisema ni haki yake na kila Mkenya kikatiba kuandamana na kushinikiza serikali kutii matakwa yao. "Ni haki yetu kikatiba kuandamana, na ndio manake naambia Wakenya wote wakuje Jumatatu kwenye maandamano," Raila alisema. 

Alitaka kuundwa kwa kamati mpya ya uchaguzi nchini IEBC kwa ajili ya 2027 kuwahusisha wote. "Kwa kamati mpya ya IEBC kuundwa ni lazima Kenya Kwanza na Azimio waketi chini na kuelewana, na pia kama wewe ulishinda fungua servers," aliongeza. 

Akizungumza Kisii, Rais William Ruto alimtaka Raila kukomesha maandamano yake mara moja na kumpa nafasi ya kuwahudumia Wakenya. Wacha kiburi. Mtu wa kubishana na mtu wa kitendawili ni mimi, badala ya kukabiliana na mimi ameanza kusumbua raia. Wewe unauliza nini Mama Mboga? Mwenye alikushinda ni mimi. 

Kama uko na shida kuja ukabiliane na mimi. Achana na mambo ya wananchi wadogo," Ruto amesema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.