ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 18, 2017

UCAF YASAINI MKATABA NA AIRTEL KUPELEKA MAWASILIANO VIJIJINI.


 Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Suingano Malya wakisaini mkataba wa Mradi wa sita wa kupeleka mawasiliano kwa wote. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini yenye lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini na hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017.
 Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Suingano Malya, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa sita wa kepeleka mawasiliano ya simu kwa wote. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini yenye lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini na hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, (kulia), akimpongeza Mwakilsh wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Malya, mara baada ya Airtel kusaini mkataba wa sita wa Mradi wa kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCAF), jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017

UCSAF wasaini makubaliano na Airtel kupeleka mawasiliano vijijini

UCSAF imesaini makubaliano na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanznia PLC  pamoja na makampuni mengine ya simu nchini kwa lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko wa mawasilano kwa wote jijini Dar es Salaam,

"Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "Airtel tunasaini mkataba huu kwa lengo la kuendelea kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma za mawasiliano kote nchini zentye ubora na ubunifu wa hali ya juu”

Singano alisema kuwa "uwepo wa mawasiliano haya vijijini utasaidia hasa kutimiza malengo mbalimbali ambayo serikali imejiwekea katika kupanua uchumi wa nchi kwa ujumla katika Nyanja mbalimbali zikiwemo elimu, afya, uboreshwaji wa shughuli za kilimo pamoja na huduma za kibenki kwa maeneo ambayo yako pembezoni mwa nchi.Tunaimani maswala ya uslama kwa watanzania waliopo mipakani yataweza kutatuliwa kwa hara na ufanisi mkubwa kupitia mawasiliano.”  

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.