JINAMIZI LA UVAMIZI WA MAENEO YA WAZI YALIYOTENGWA KWA AJILI YA UKUZAJI WA VIPAJI KWA VIJANA HUSUSANI MICHEZO LIMEENDELEA KUTAFUNA MAENEO KWA MAENEO NA SAFARI HII LIMEGEUKIA KIWANJA CHENYE HISTORIA YA KUTOA WASUKUMA KANDANDA MAARUFU NCHINI MUHIMU KWA TAIFA WALIOTAMBA ZAMANI AKINA MBUYI YONDANI,MZEE HALFANI NGASA, HAMADI BILIYOMO(RTC MZ+TOTO) NA WAKALI WA SASA JERRY TEGETE, NGASA,HENRY JOSEPH NAWENGINEO WENGI. NAUZUNGUMZIA UWANJA WA FURAHISHA ULIOKO KIRUMBA JIJINI MWANZA. WAKATI MHESHIMIWA RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIPIGANA KUFA NA KUPONA KUONA TAIFA LINASONGA MBELE KATIKA NYANJA YA MICHEZO SAMBAMBA NA KUHAKIKISHA KUWA WATU WAKE WANAPATA MISINGI BORA TANGU AWALI KATIKA HATUA ZA KIMICHEZO KUTIMIZA AZMA, TIZAMA HILI LINALOFANYIKA SASA KATIKA ENEO LA WAZI LA UWANJA WA MICHEZO FURAHISHA KIRUMBA JIJINI MWANZA, AMBAPO HALMASHAURI YA JIJI IMEMEGA SEHEMU YA UWANJA HUO KUWA DAMPO. SI MICHEZO PEKEE ITAKAYOATHIRIKA VIPI KUHUSU AFYA ZETU NA WATOTO WETU? KWANI TAKA HIZI ZIKO KATIKA UWANJA HUU ULIO KARIBU KABISA NA NAKAZI YA WATU. ETI ENEO HILI NI KWA KUKUSANYA TAKA TU!. NANI KASEMA? KWA MUJIBU WA WAKAZI WA ENEO HILI MKURUGENZI WA JIJI BW. WILSON KABWE NDIYE ALIYE IDHINISHA HILI KUFANYIKA HAPA. SHULE NYINGI ZA MWANZA MFANO. SHULE YA MSINGI MILONGO JUU, SM KITANGILI, SM. NYAMAGANA, HATA SHULE YA SEKONDARI LAKE HAKUNA VIWANJA, WATOTO WENGI WANACHEZA KWENYE MAWE VIWANJA VYA MICHEZO MASHULENI VIMEJENGWA MADARASA AU OFISI. SASA NI ZAMU YA HIKI TAAAARATIBU TUNAPIGA FENSI KESHO INSHU NYINGINE HAPA HAPA. WAKIWA MAKUNDI KWA MAKUNDI NDEGE HAWA KWA HIVI SASA ENEO HILI LIMEKUWA YAO MAKAZI.
”Rasmi Soko Kuu la Manispaa ya Bukoba lavunjwa”
-
Soko Kuu la Manispaa Bukoba limevunjwa ili kupisha ujenzi wa soko jipya la
kimataifa unaotarajiwa kuanza muda wowote.
Kwa Wakati tofauti wameonekana Wafa...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.