JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB imewatia mbaroni watu watatu ambao wanadaiwa kuiba kiasi cha Sh700 milioni kwa nyakati tofauti. |
Watuhumiwa hao wamenaswa baada ya kuwekewa mtego na maofisa wa benki na polisi kwenye saa 6.00 usiku wa Februari 10, mwaka huu na mtuhumiwa mmoja alibambwa akichukua fedha katika ATM ya NMB kwenye Tawi la PPF Plaza Mwanza.
Baada ya kunaswa kwa mtuhumiwa huyo, alisaidia
kuwaelekeza polisi walipo wenzake, ambao walikutwa katika hoteli moja jijini
Mwanza wakiwa wamejipumzisha.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza, Christopher Fuime alisema pia walikamata vifaa mbalimbali ambavyo walikuwa wakitumia kwa ajili ya kufanyia uhalifu huo. |
Mbali na kadi hizo pia waliweza kunasa kadi 36 za Benki
za DTB, ambazo kati yake kadi 18 zilikuwa na jina moja la Kelvin G. Gratias na
namba 20497883, kadi 12 zikitumia jina la John J. Paul zenye akaunti namba
2049783 huku kadi sita zikitumia jina moja la Joseph Donald akaunti namba
2049783.
Kadi nyingine tatu zenye maandishi ya Download List na
nyingine ikiwa ni kadi ya Visa ya Benki ya KCB yenye namba 4183546040003827
zikitumia jina la Elikana Zacharia. Kadi nyingine zilikuwa ni tupu zisizo na
maandishi wala nembo ya benki yoyote na nyingine zikiwa ni Soviet Royalty, kadi
ya raia ya Urusi ikiwa na namba 000724.
Pia walikutwa na kadi ya Benki ya Amerikani yenye namba 549012345678 zilizokuwa zikitumia jina la Richard Croswell. |
Walikamatwa pia wakiwa na vifaa mbalimbali vya kielektroniki
ikiwamo kamera za siri tatu za kienyeji ambazo zimetengenezwa kwa kufungwa
betri za simu ya mkononi na pia walikamatwa na kifaa cha kutengenezea kadi
bandia (Magnetic Card reader), mikebe mitatu ya rangi za kupulizia kamera za
usalama katika ATM ili wasionekane wakati wa wizi wao, ‘printer’ pamoja na
kifaa cha kuchomea vifaa vya umeme.
Mara baada ya kuziharibu kamera za usalama, walikuwa
wakianza kwa kuweka kamera zao za siri ili kunasa namba za siri za kufungulia
akaunti ambazo huzisoma katika ‘kompyuta’ na kuzinakili katika daftari lao
maalumu na kisha kuchukua kadi zao bandia na kuchukua fedha.
Wizi huo wa kuchukua fedha waliufanya nyakati za usiku
saa sita hadi saa tisa usiku wakati ule wa kutegea kamera zao ulifanyika muda
ambao huwa na wateja wengi hasa siku za mapumziko.
Tupe maoni yako
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDelete