Mabondia wanaotaraji kupambana katika mapambano mawili ya IBF yanayofanyika katika majiji ya Johannesburg na Tunis, leo wamekamilisha kupima uzito kabla ya kuingia ulingoni.
Mapambano haya yaliyopewa jina la “Barabara ya kutoka Cape Town mpaka Cairo kwa IBF” kutokana na majiji haya kukaa moja kusini na lingine kaskazini mwa Afrika, yanafanyika wakati IBF ikijipambanua vyema katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Kusini mwa Afrika, leo imeshughudia mabaondia mawili wanaopambania ubingwa wa dunia kwa vijana walio chini ya miaka 25 wakipima uzito mbele ya mashirika mbalimbali ya habari ya ndani na nje ya Afrika ya Kusini.
Illunga Makabu kutoka Jamhuri ay Watu wa Kongo (DRC) alipima uzito kumkabili Gogota Gorgiladze wa Georgia. Upimaji huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa ulio katika hotel ya nyota tano ya Emperors Palace iliyoko katika jiji la Johannesburg!
Rodney Berman mtu anayeheshimika kwa kuwa promota wa kwanza kuandaa pambano la IBF la dunia katika bara la Afrika mwaka 1990, ndiye anayepromoti pambano hili!
Tayari wadau na mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika zikiwamo Namibia, Zambia, Msumbiji, Zimbabwe na Tanzania wameshawasili nchini Afrika ya Kusini tayari kuangalia mpambano huo. Wengine walibaki Afrika ya Kusini wakati wa mashindano ya kombe la Afrika yaliyomalizika wiki iliyopita.
Kaskazini mwa Afrika,
Bondia ambaye ameshajizolea sifa kemkem Ayoub Nefzi wa Tunisia anayeishi nchini Belgium atapigana na bondia Ishmael Tetteh kutoka nchi ya Ghana kugombea ubingwa wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika uzito wa Light Middle.
Mpambano huo uliopewa jina la “Uzuri wa Jasmine” kutokana na jina hilo kutumika katika mapinduzi yaliyomwondoa Rais wa zamani wa Tunisia Ben Ali unafanyika wakati Ayoub Nefzi akijiandaa kugombea mkanda wa juu wa IBF wa mabara mwezi wa tatu nchini Belgium.
Mabondia wote wawili wanatagemea kuonyesha moto mkali katika mpambano ambao tayari mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi za Nigeria, Ghana, Libya, Misri, Algeria tayari wameshawasili nchini Tunisia kuangalia mpambano huo!
Tunisia inasifika kama nchi iliyowahi kutoa viongozi wengi wa mchezo wa ngumi katika bara la Afrika.
Imetolewa na:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.