“Nawashukuru viongozi wa mkoa wa Mwanza kwa kuwezesha kuja kutambulsha kitabu hiki baada ya uzinduzi wake Dar es salaam, ni heshima ambayo mlistahili na hasa nikikumbuka vile mlivyoandaa sherehe zile za Uhuru 9 Disemba mwaka jana (2019), zikafana sana pamoja na nyimbo za kwaya ile, nasema hii ni heshima kubwa kwangu. Hongereni sana kwa matayarisho ninyi ni hodari sana” Asema Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin W. Mkapa katika hafla ya utambulisho wa kitabu chake 'MY LIFE, MY PURPOSE' uliofanyika ukumbi wa Hotel Malaika jijini Mwanza. “Kwanini niliamua kuandika kitabu hiki? Ni kwasababu ninalaumiwa sana katika jamii hasa wanasiasa kutokana na sera nilzokuwa nikizitekeleza wakati wa uongozi wangu” “Ninasemwa kuwa mtu jeuri, najiona sana, sasa n jukumu lenu someni kile kitabu halafu muamue kweli huyu ni jeuri” “Kuna dhana inayosemwa kwama Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliniandaa toka mwanzo ili nije kuwa rais wa nchi, HII SI KWELI” Amesisitiza Mhe. Mkapa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.