NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amewahimiza wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika kushiriki zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la makazi kwa ajili ya kumwezesha kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Koka ameyasema hayo wakati alipokwenda kutimiza haki yake ya msingi ya kwenda kujiandikisha katika daftari hilo katika ofisi ya serikali ya mtaa kituo cha Mkoani 'A'
Aidha Koka mbali na kujiandikisha alitumia fursa ya kuweza kuzungumza na wananchi mbali mbali na kutoa hamasa juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari hilo.
"Leo nimeweza kushiriki kikamilifu katika zoezi la kujiandikisha na nimeungana na wananchi wangu na kutoa hamasa waweze kujiandikisha "alifafanua Mbunge Koka.
Aidha Mbunge huyo alifanya ziara ya kutembelea vituo vya kujiandikishia ambapo amedai mwamko wa wananchi ni mzuri na kuwahimiza waendelee kujitokeza.
Mbunge huyo aliweza kutembea kwa miguu na kupita maeneo kadhaa likiwemo la stendi ya Loliondo,Soko la mnarani na kuwatembelea wafanyabiashara wa bidhaa mbali mbali na mafundi magari.
Koka aliwahiza wananchi kutofanya makosa na kuhakikisha kwamba wanamchagua viongozi mwenye sifa na uwezo ambaye ataweza kusikiliza changamoto zao na kuwaletea chachu ya maendeleo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.