MWANDISHI NA. VICTOR MASANGU/PWANI
SAUTI NA. ALBERT G.SENGO
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja ambaye anadaiwa kuhusika katika kutengeneza picha za mjongeo za utupu zenye maudhui machafu ambayo ni kinyume kabisa na maadili na sheria za nchi na kuamua kuzisambaza katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Salim Morcase amesema kwamba mtuhimiwa huyo baada ya kufanya uchunguzi na kwamba alitengeneza picha hizo za utupu kwa kutengengeneza na kuunganisha na baadhi ya picha za majengo ya shule ya sekondari Baobab kwa lengo la kuaminisha umma kuwa vitendo hivyo vimefanyika shuleni hapo kitu ambacho sio cha kweli hata kidogo.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shule ya sekondari Baobab Shani Swai amekanusha vikali na kusema kwamba kwamba wamesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya watu kuamua kuwachafua taasisi yao kwa kusamabaza picha hizo za utupu katika mitandao ya kijamii na kusababisha kuleta hali ya sintofahamu na taharuki kubwa katika maeneo mbali mbali hasa kwa wazazi na walezi.
Naye Kaimu mkuu wa shule taalamu Alphonce Kamisa na Mwenyekiti wa Bodi ya Talaamu wa shule ya hiyo wamesema kutokana na jambo hilo limeweza kuleta taharuki kubwa licha ya kwamba wanafunzi tayari wamesharipoti shule kwa ajili ya kuanza na masomo yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.