ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 12, 2016

TATHIMINI UNGWE YA KWANZA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA 2016-2017

VIDEO KILICHOJIRI japo uduchu ndani ya kipindi cha KIPENGA

Time yako asubuhi hii kukutana nasi kispoti zaidi #KIPENGA ndicho kipindi ukiwa na @jumaayoo @elikanamathias featuring wachambuzi wa siku ya leo ni @salehjembe na wakali wengine. Majogoli kuhusishwa kama kawa safari hii tunatua pale mjini Shinyanga na kisha tunapaa hadi jijini Dar es Salaam ndani ya Club ya Azam FC suala la kukuza vipaji #VeePe!!?!! Tupate popote ulimwenguni kupitia Google play store kwa kusachi JEMBE Fm HD kisha sikiliza LIVE kupitia simu yako ya mkononi AU nenda kwenye TUNe in search JEMBE FM aksante kwa kutusikiliza. @djscopion

CHANZO/GAZETI LA CHAMPION 
...Nahodha wa Simba, Jonas Mkude, ameonyesha ukomavu kwa kusema licha ya timu yake kupoteza mechi mbili mfululizo, bado hawajakata tamaa na nia yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara iko palepale.

Simba ipo kileleni mwa ligi kuu ikiwa na pointi 35 lakini imepoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya African Lyon (bao 1-0) na Prisons kwa mabao 2-1 kabla ya ligi hiyo kusimama.

Katika mechi 15 za ligi, Simba imeshinda 11, imetoka sare mbili na kufungwa mbili, Mkude amesema takwimu hizo haziwezi kuwatoa katika mbio za ubingwa msimu huu.

Kiungo huyo amesema kuwa, kupoteza mechi mbili ni sehemu ya mchezo lakini wameshabaini makosa yao waliyoyafanya na baada ya mapumziko watayafanyia kazi na kurudi tena katika moto wao.

“Tumefungwa kwa sababu huu ni mchezo ambao una matokeo matatu na tumepokea matokeo haya na hatuna budi kukazana kwenye mechi zijazo kuhakikisha kwamba hatupotezi kama ilivyotokea kwenye mechi hizi mbili za mwisho.


“Hatujakata tamaa kutokana na kufungwa kwani ndiyo kwanza vipigo vimetuamsha zaidi na tutajitahidi kupambana kwa kila hali katika mzunguko wa pili tufanye vizuri,” alisema Mkude.


Mwadui FC sasa ipo chini ya Khalid Mohammed ambaye ametamba timu yake kutisha katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Mohammed amechukua nafasi ya Jamhuri Kihwelo 'Julio' ambaye 'alikimbizwa' na waamuzi wasiotenda haki.

Mohammed amesema wakati huu ambapo ligi imesimama, amewapa mapumziko mafupi vijana wake kisha watarejea kwa mazoezi makali kambini kwao na ana imani watafanya vizuri mzunguko wa pili.

Mwadui ipo katika nafasi ya 15 katika ligi ambayo si nzuri ikiwa na pointi 13 katika mechi 15 ilizocheza ambapo imeshinda tatu, imetoka sare nne na kufungwa mara nane.

Mohammed amesema kuwa: “Unajua siyo kila msimu timu inakuwa na matokeo mazuri, hii hali inaweza kuitokea timu yoyote ile, sasa tunaenda kujipanga.


“Katika kikosi kuna upungufu mdogo nimeubaini, hasa kwenye kiungo na ulinzi, tutakitumia kipindi kijacho cha usajili wa dirisha dogo kuimarisha kikosi, naamini mzunguko wa pili tutakuwa vizuri.”

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.