HATIMAYE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEMTEUA MH. MIZENGO PINDA MBUNGE WA JIMBO LA KATAVI, KUWA WAZIRI MKUU KWA AWAMU NYINGINE. SPIKA MPYA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. NDANI YA UKUMBI WA BUNGE MH. ANNA MAKINDA ALIFUNGUA BAHASHA NA KUISOMA BARUA TOKA KWA MH. RAIS IKIMTAJA PINDA KUWA NDIYE.
KUPITIA KURA ZA PAPO KWA HAPO TAYARI WABUNGE WAMEMTHIBITISHA WAZIRI MKUU HUYO AMBAPO MWANASHERIA MKUU MH. FREDERICK WEREMA AMESOMA MATOKEO YA KURA KAMA IFUATAVYO:- KURA ZILIZOPIGWA 328, ZILIZOHARIBIKA 2 SAWA NA ASILIMIA 0.6 KURA ZA HAPANA 49 SAWA NA ASILIMIA 14.9, KURA ZA NDIYO NI 277 SAWA NA ASILIMIA 84.5.
WAZIRI MKUU ANATARAJIWA KUAPISHWA KESHO IKULU NDOGO YA CHAMWINO, IKIWA NI HATUA YA KWANZA KABLA YA KUTANGAZWA KWA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI. HATUA HII INAKAMILIKA BAADA YA RAIS KUKAA NA KUSHAURIANA NA MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU.
BARAZA HILO JIPYA LINATARAJIWA KUTANGAZWA IJUMAA.......
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akiteta na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na aliyekuwa Mbunge wa Karatu kabla ya uchaguzi (oct 2010), Dr. Wilbroad Slaa kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma, Aprili 13, 2010. Bunge lilihamia katika ukumbi huo baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya wa Bunge kupata hitilafu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.