ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 6, 2016

MKUU MPYA WA MKOA WA MWANZA USO KWA USO NA WAANDISHI WA HABARI

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amewaomba waandishi wa habari jijini Mwanza kushirikiana na serikali ya mkoa Taasisi mbalimbali katika kuutangaza mkoa katika nyanja mbalimbali za uwekezaji, utalii, biashara, kilimo na uvuvi ili ukue kiuchumi na kimaendeleo.
Sehemu ya waandishi wa habari waliojitokeza kumsikiliza mkuu huyo.
Mwanahabari Nashon Kennedy kutoka Daily News akichangia kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Sehemu ya wanahabari.
Peter Fabian mwandishi wa habari kutoka gazeti la Mtanzania akifunguka namna ya ushirikishwaji wa waandishi katika kuusaidia umma wa wananachi wa Mwanza kupata elimu itakayowakwamua kuziona kwa jicho la ziada fursa za uwekezaji zilizopo jijini Mwanza.
Sehemu ya wanahabari waliojitokeza kwenye kusanyiko hilo.
Kwa umakiiiiini.
Pointi = Wanahabari wako tayari kushiriki zoezi husika lakini changamoto kuu ni uwezeshwaji pamoja na vitendea kazi, kama mkoa utaamua kuwekeza kwa waandishi kuzibaini changamoto zao na kuzitatua naam tutegemee kuona matokeo chanya.
Sitta Tuma.
Fredrick Katulanda na Mseti.
Vinasio na uchukuaji wa taarifa.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza amesema anahitaji ushirika mzuri na waandishi wa habari katika kubaini na kukabiliana na wimbi la uhalifu kwani kupitia wao i rahisi kupata taarifa za waharifu. 
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.