ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 7, 2016

MCHEZAJI KANU WA NIGERIA AZINDUA DUKA JIPYA LA STARTIMES KESHO KWENDA KUTEMBELEA SHULE YA MSINGI MAJIMATITU MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM


  Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (kulia),akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la Kampuni ya StarTimes lililopo jengo la Mkuki Mall Barabara ya Nyerere Dar es Salaam leo mchana. Mchezaji huyo yupo nchini kwa ziara ya siku tano. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao.
 Ofisa Mauzo wa StarTimes Tanzania na mshereheshaji wa uzinduzi huo, Tang Jing Yu 'Juma Shorabaro wa Kichina'  (kulia), akiendelea na majukumu yake.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Mr.Canter, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (wa pili kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

 Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaamleo mchana, baada ya kuzindua duka la Kampuni ya StarTimes lililopo jengo la Mkuki Mall wakati wa ziara yake aliyoianza jana  nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Mr.Canter, Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao, Katibu wa mchezaji huyo, Kingstey Obiekwe na Makamu wa Rais wa StarTimes, Zuhura Hanif.
  Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (katikati), akitia saini yake katika jezi.
 Kanu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa StarTimes na wa jengo la Mkuki Mall baada ya kuzindua duka hilo.
Mmiliki wa Blog ya Full Shangwe, John Bukuku akichukua picha na mchezaji huyo.

Na Dotto Mwaibale


Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Naijeria (Super Eagles) na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu ameshiriki katika uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya StarTimes Tanzania lililopo katika jengo la Mkuki Mall Barabara ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mchezaji Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika ambapo inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya 10 amesema kuwa anajisikia mwenye furaha kuwepo nchini na atashiriki shughuli mbalimbali za kampuni pamoja na za kijamii.

“Ni mara ya kwanza mimi kuwepo nchini Tanzania, nashukuru nimefika salama na kupokelewa kwa ukarimu mkubwa, kwa kweli sikutarajia. Uwepo wangu hapa ninaiwakalisha kampuni ya StarTimes barani Afrika kama balozi wao na kama balozi ninao wajibu wa kufika kila nchi ambayo kampuni hii ipo. Kwa namna nilivyopokelewa ninaamini kuwa kweli StarTimes ni kampuni kubwa, inapendwa na kujulikana miongoni mwa watanzania wote.” Alielezea Bw. Kanu

“StarTimes wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanafurahia huduma za matangazo ya dijitali kwa ubora wa hali ya juu na gharama nafuu. Na hii ni kutokana na falsafa iliyojiwekea kampuni ya kutaka kuhakikisha kuwa kila nyumba ya muafrika inafikiwa na matangazo hayo. Changamoto ni nyingi katika uendeshaji na utoaji huduma za kidijitali lakini kampuni imejizatiti kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika uboreshaji wa vipindi na chaneli zake. Kwa mfano kwa sasa kama mnavyoweza kushuhudia kuwa ligi kubwa barani Ulaya za Bundesliga na Serie A za nchini Ujerumani na Italia zinaonyeshwa moja kwa moja kupitia StarTimes Pekee.” Aliongezea Kanu

“Michezo na burudani ni maudhui muhimu sana ambayo lazima yawekewe mkazo kwani ndivyo vitu vinavyopendwa na kuwavutia wateja wengi hivyo haina budi kuweka mkazo. Ninaamini kuwa uwepo wangu nchini Tanzania utasaidia kwa kukaa chini na uongozi wa kampuni nchini na kuweza kuona wanawaongezea na kuwapatia nini wateja wao. Ninatumaini ninacho cha kuongezea kwa nilichojifunza kutoka nchi kama za Uganda na Kenya ambazo nimetokea huko pia,” alisema na kumalizia Kanu kuwa, “Nashukuru kuwepo Tanzania na ninaamini nitajifunza na kushirikiana kwa mengi kwa kipindi nitakachokuwepo mpaka kuondoka kwangu.”

Naye kwa upande wake akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya ambalo litakuwa ni la saba kwa mkoa wa Dar es Salaam pekee, Mkurugenzi wa Uendeshaji (Operesheni) wa StarTimes Tanzania, Bw. Carter amebainisha kuwa duka hilo jipya litawarahishia wateja wote wanao kama maeneo ya jirani kama vile Tandika, Mbagala, Temeke, Kurasini, Yombo, Kiwalani, Vingunguti na kwengineko kujipatia huduma na bidhaa kwa urahisi zaidi.

“Leo tunayo furaha kubwa kufungua duka hili jipya ambalo katika kumbukumbu litakuwa limezinduliwa na balozi wetu barani Afrika, Nwanko Kanu. Duka hili litakuwa msaada mkubwa kwa wateja walio maeneo ya jirani na kwingineko na ningependa kuwatoa wasiwasi kuwa litakuwa linatoa huduma zenye ubora sawa na maduka yetu yote hivyo wasiwe na wasiwasi. Ninawaomba wateja wetu watembelee hapa kujipatia huduma kama vile kununua visimbuzi, antena na kebo, vocha za malipo ya mwezi pamoja na huduma kwa wateja.” Alimalizia Bw. Carter.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.