Siku meya mpya wa jiji la Mwanza kupitia CHADEMA Bw.Josephat Manyerere(kulia) aliposhinda na kupongezwa na mbunge wa Nyamagana Mh.Wenje, na kwa chati pembeni ndiye marehemu diwani wa Mwaloni Kirumba Bw.Novat Manoko....
Mwili wa diwani huyo leo ulichukuliwa toka hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa maandamano makubwa ya vijana waliokuwa wakipeperusha bendera za chama hicho huku ummati wa waandmanaji ukiongezeka hatua kwa hatua kuelekea nyumbani kwa marehemu ambapo msiba utakesha pale kwaajili ya shughuli za heshima ya mwisho hapo kesho.
Moja kati ya kashikashi alizowahi kukutana nazo marehemu katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa mwaka jana uliompatia ushindi ni tukio lililotokea mnamo september 2010 kunusurika kufa baada ya kuvamiwa na kukatwa mapanga na watu wasiojulikana ambapo katika tukio hilo, Manoko alijeruhiwa sehemu za kichwani.
Marehemu pia alikuwa mkuu wa wafanyabiashara katika soko linaloshika Uchumi wa jiji la Mwanza, Mwaloni Kirumba.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.