
Akikabidhi msaada huo Mabula amesema kwamba yeye akiwa kama mdau wa michezo ametekeleza ahadi yake ya kuchangia timu hiyo baada ya kuombwa na uongozi wa timu hiyo kama sehemu ya chachu ya timu hiyo inayoshiriki ligi ya wilaya ya Ilemela na michuano ya kombe la ng’ombe inayoendelea kwenye uwanja wa michezo wa Jeshi Nyegezi ambapo timu hiyo imetinga hatua ya robo fainali.
Ameongeza kuwa akiwa kiongozi wa wananchi wa kata ya Mkolani na mdau mkubwa wa michezo ataendelea kutoa misaada mbalimbali ambayo italenga kukuza vipaji na kuendeleza michezo na amewaomba viongozi wengine wakiwemo na viongozi wenzake kuendelea kuzisaidia timu mbalimbali badala ya kuliachia jiji pekee ambalo huchukuwa muda mrefu kupitisha fedha za kuzisaidia timu na vifaa hali inayosababisha timu zetu kutofanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali zinazoshiriki.

“Uongozi ni kuonyesha mfano na kuhakikisha unasimamia maendeleo kwa jamii ili kuleta manufaa ambayo yatasaidia vijana kukuza vipaji, kupata ajira na kuendeleza sekta ya michezo kwa kuzingatia ilani zilizo wekwa kuendeleza michezo nchini, jinsi zinavyotekelezwa kwa vitendo basi zinakuza kwa watu walio wachagua” Alisema Mkurugenzi kabwe wakati akitoa shukurani.

Wakati akikabidhi vifaa hivyo na fedha Diwani Mabula amesema kwamba mwaka huu mashindano hayo ya Kamanda Cup atayabadilisha jina na kuitwa Mkolani Cup na yatashirikisha timu kutoka mitaa yote ya kata hiyo, huku akiwa ameyaboresha zaidi kwa kutoa vifaa vya michezo vyenye ubora na kuongeza fungu kubwa kwa upande wa zawadi hivyo amezitaka timu kuanza maandalizi mapema ikiwemo Fc Shadia ambayo tayari imepata changamoto ya vifaa vitakavyoisaidia timu hiyo kwenye maandalizi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.