"Si wakati wa kukata tamaa ni wakati wa kufarijiana kushikamana na kusema kurudi nyuma mwiko" Mbunge wa Musoma mjini Vicent Makongoro akihutubia wananchi waliokusanyika katika viwanja vya Magomeni kirumba jijini Mwanza kwaajili ya kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.
"Ndugu zangu Leo tumesimama hapa hatupo katika kujali chama bali tupo kwa ajili ya kazi na mema aliyofanya ndugu yetu aliyelala ambaye namfahamu sana tangu nikiwa naibu meya wa jiji la Mwanza yeye akiwa mkusanyaji mzuri wa mapato ya Halmashauri na kwautendaji wake alikuwa rafiki yangu mzuri sana" Kauli ya Mbunge wa CCM Mama Maria Hewa ambaye aliyeshangiliwa na umati uliofurika viwanjani hapo mara baada ya kutoa salamu ya PEOPLE'S ......
Mbunge wa Ilemela Mh. Highness Samson akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Diwani Novatus Manoko.
Mbunge wa Nyamagana Mh. Wenje akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu N. Manoko.
Kwaheri KIONGOZI ndivyo alisikika akisema mama huyu mwanachama wa CHADEMA.
Kulikuwa na misafara ya mistari minne kutoa fursa kuelekea kuaga mwili wa marehemu.
Akina mama wafanyabiashara wa soko la Mwaloni Kirumba katika sare ya pamoja.
Usimamizi ulidhibitiwa kumwezesha kila mwananchi kufika eneo la tukio.
"R.I.P Kamanda"
Sehemu ya wana ndugu na familia ya marehemu.
Umma
Hatimaye jioni ya leo marehemu amezikwa katika makaburi yaliyoko eneo la Kitangiri kata ya Kirumba wilayani Ilemela jijini hapa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.