Mbio za km 21 kwa upande wa wanawake Jackline Juma toka mkoani Arusha ameibuka mshindi na kuzawadiwa shilingi laki 5, mshindi wa pili Natalie Elisante (Ar) shilingi laki 3 na aliyeibuka nafasi ya 3 ni Sara Maja wa Kilimanjaro aliyejinyakulia shilingi laki 2, mshindi wa 4 hadi wa 10 wameondoka na kifuta jasho cha shilingi elfu 90 kila mmoja.
Mbio za km 5 zilizo kuwa na washiriki 35 upande wa wanaume, Mohamed Dole toka Arusha ameibuka nafsi ya kwanza, Doto Ikangaa nafsi ya pili akitokea Arusha na nafasi ya tatu imetwaliwa na mshiriki kutoka mkoa wa Singida Paschar Ramadhani.
Wanawake km 5 zilizokuwa na washiriki 21, mshiriki kutoka mkoani Mara Veronika Titus ameibuka mshindi wa kwanza, mshindi wa pili Neema Maiko na watatu Hawa Hezebin toka Mwanza.
Mbio zilizo tia fora nia za km 3 kwa Wazee ambapo washiriki walikuwa 18 wote wakijinyakulia mkwanja wa shilingi elfu 25 kila mmoja . Mshindi wa kwanza katika mbio hizo akiwa mzee Stanslaus Mahane, wa pili mzee Elias Kagoma na wa tatu mzee Mohamed Wawa wote kutoka Mwanza.
Macho ya wengi yalizama kwenye mbio za washiriki walemavu wa ngozi zilizokuwa na washiriki 11 ambapo wote walizawadiwa shilingi elfu 25 kila mmoja, zilizoshuhudia Maneno Enock wa Mwanza akiibuka mshindi nafasi ya kwanza, Fadhili Marko (Mz) akiinyakua nafasi ya pili naye Japhet John (Mz) kuambulia nafasi ya tatu.
Kauli mbiu ya Rock city Marathon 2011 ni TUTANGAZE UTALII KUPITIA MICHEZO.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.