Mamlaka
nchini Nigeria, zimesema washukiwa wa kundi la kijihadi la Boko Haram,
wametoweka katika gereza la Kuje, jijini Abuja, baada ya watu wenye
silaha kuvamia gereza hilo, usiku wa kuamkia leo.
Hata hivyo
mamlaka nchini humo hazijasema idadi wa washukiwa waliotoweka wakati wa uvamizi
huo, ambao jeshi la Nigeria limesema lilifanikiwa kuuthibiti.
Kwa miaka ya
hivi karibuni makundi ya kijadi yamekuwa yakivaimia magereza nchini Nigeria,
zaidi ya wafungwa 5,000 wakifakiwa kutoroka tangu mwaka 2020.
Tukio hili
limejiri muda mfupi baada ya watu wenye silaha kushambulia msafara wa rais Muhammadu
Buhari, kaskazini mwa taifa hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.