Polisi
nchini Nigeria wameanzisha msako kuwatafuta mapadri wawili wa kanisa katoliki
waliotekwa mwishono mwa juma, katika jimbo la Edo.
Mapadri hao
Udo Peter na Philemon Oboh, walitekwa na watu wenye silaha katika barabra kuu
ya Benin- Auchi.
Kisa hiki
kinajiri siku chache baada ya watu wenye silaha kumteka na kumuua padri
mwingine Christopher Odia, karibu na mji wa Auchi.
Katika hatua
nyingine mamlaka katika jimbo la Zamfara, kuko huko nchini Nigeria zimesajili
vijana 9, 000, ambao wamejukumiwa kulinda jamii na kupambana na majambazi.
Mwishoni mwa
mwezi uliopita gavana wa zamfara, Bello Muhammad, aliwataka raia kununua silaha
ili kujilinda dhidi ya uvamizi wa makundi ya watu wenye silaha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.