ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 5, 2022

WANAFUNZI 10 BORA MASOMO YA SAYANSI KIDATO CHA SITA 2022 HAWA HAPA.

matokepoiicc 

Kaimu Katibu wa Baraza Hilo, Athuman Amas amemtaja Catherine Alphonce Mwakasege kutoka shule ya St.Mary's Mazinde Juu kuwa kinara wa matokeo hayo katika masomo ya sayansi mchepuo wa PCB.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Lucy E Magashi kutoka shule ya St. Mary's Mazinde Juu Tanga kutoka PCB. Muhewa Charles Kamando kutoka Tabora Boys, PCB akishika nafasi ya tatu akifuatiwa na Minael Simon Mgonja kutoka St.Mary's Mazinde Juu mkoani Tanga PCB, aliyeshika nafasi ya nne.

Nafasi ya tano imechukuliwa na Norah Eliaza Kidjout kutoka shule ya St.Mary's Mazinde Juu (Tanga) PCB, akifuatiwa na Jennifer Martin Chuwa aliyeshika nafasi ya sita kutoka St Mary's Mazinde Juu, PCB.

Pauline Ildephonce Mabamba kutoka St.Mary's Mazinde Juu Tanga PCM akichukua nafasi ya saba, Rachel Joachim Moshy amechukua nafasi ya nane kutoka St.Mary's Mazinde Juu Tanga, akichukua mchepuo wa PCM.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.