ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 5, 2022

KIKOPE NI NINI? Sababu, matibabu na kuzuia tatizo la kuvimba kope (sekela)

 Kikope (stye) ni uvimbe mwekundu unakuwa juu au ndani ya ukingo wa kope ya jicho lako, uvimbe huu unaouma huwa unaaanza kuvimba na kuongezeka ukubwa ndani ya siku kadhaa.

Uvimbe huu huw unatokana na maambukizi ambayo huwa yameanzia kwenye shina la unywele wa kope . Inaweza ikawa ngumu kufungua jicho au unaweza kuanza kujihisi kama kuna kitu ndani ya jicho, hasa unapo fumba na kufungua jicho. Jicho lako linaweza kuwa linatoa machozi na mwanga unaweza kuwa unakuumiza ukiuangalia. Kikope huwa kinakua na baadae kinapasuka, kinapopasuka maumivu huanza kupungua, japo kuna baadhi ya vikope huwa vinaisha tu vyenyewe hata kabla ya kupasuka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.