ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 8, 2022

WATEMI SHINYANGA WASISIMUA TAMASHA LA BUSIYA SABA SABA KUNADI LUGHA YA KISWAHILI

Kamisaa wa Sensa Taifa Anna makinda Amezindua Tamasha la Utamaduni La Sanjo ya Busiya(7SabaFEST) wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.. Makinda ametumia Tamasha hilo kuhamasisha wakazi wa mkoani Shinyanga kujitokeza kuhesabiwa Itakapofika August 23 ili Serikali iweze kujua idadi ya watu wake na kusaidia kuleta maendeleo..

Tamasha la Sanjo ya Busiya hufanyika kila mwaka na kilele chake ni Tarehe 07/07/2022 na kauli mbiu ya Mwaka huu "Watu wote wahesabiwe Tuwe na Takwimu sahihi kwa maendeleo Yetu'

Maelfu ya Watu wakusanyika Tamasha la Sanjo ya Busiya (7SabaFEST) Ikiwa ni kilele cha siku ya kiswahili Duniani pamoja Kilele cha sherehe za sanjo ya Busiya wilayani kishapu mkoani shinyanga  ,Ntemi wa Busiya Edward Makwaia ametumia Tamasha hilo kuwataka watanzania kukitunza na kukienzi kiswahili kwani ni Lugha ya taifa  pia ni alama muhimu inayotambulisha utamaduni wa mtanzania.
Salaam salaam.
Tuzo na medali za Rais samia Suluhu zatolewa kwa washindi wa Tamasha la utamaduni kitaifai kutoka Utemi wa Busiya Shinyanga.
Tuzo na medali za Rais samia Suluhu zatolewa kwa washindi wa Tamasha la utamaduni kitaifai kutoka Utemi wa Busiya Shinyanga.
Washiriki wa shindano la mavazi asili.
Ntemi wa Busiya Edward Makwaia.
Ngoma imebamba.
Tamasha limenoga.
Dawa asili nazo zilikuwepo tamashani.
Ntemi wa Busiya Edward Makwaia akipata maelezo kutoka kwa waratibu.
Piza za juu kwa juu.
Kusanyiko likifuatilia yanayojiri tamashani.
Ze engo.
Maelfu ya Watu wakusanyika Tamasha la Sanjo ya Busiya (7SabaFEST) Ikiwa ni kilele cha siku ya kiswahili Duniani pamoja Kilele cha sherehe za sanjo ya Busiya wilayani kishapu mkoani shinyanga  ,Ntemi wa Busiya Edward Makwaia ametumia Tamasha hilo kuwataka watanzania kukitunza na kukienzi kiswahili kwani ni Lugha ya taifa  pia ni alama muhimu inayotambulisha utamaduni wa mtanzania.
 
Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.